GET /api/v0.1/hansard/entries/1032591/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1032591,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1032591/?format=api",
"text_counter": 130,
"type": "speech",
"speaker_name": "Laikipia North, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Sara Korere",
"speaker": {
"id": 13134,
"legal_name": "Sara Paulata Korere",
"slug": "sara-paulata-korere"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika, nilibahatika kuwa katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Afya jana, ambapo madaktari waliwasilisha malalamishi yao. Inasikitisha kwamba katika Bunge hili, kila mmoja wetu hapa anajua rafiki, ndugu au jamii ambaye ameangamia kutokana na makali ya virusi vya Korona. Hata kuna wenzetu katika Bunge hili ambao wameangamia. Tulivyo keti hivi, tunaangaliana kama “marehemu watarajiwa” manake hatujui nani atafuata. Najua Wabunge wanasikitika na kushtuka sana ninaposema sisi ni “marehemu watarajiwa” lakini Waswahili husema ukiona mwenzako ananyolewa, tia chako maji. Rais amefanya yote awezayo. Ni muhimi Waheshimiwa katika Bunge hili kumuunga Rais mkono, haswa katika vita dhidi ya ufisadi."
}