GET /api/v0.1/hansard/entries/1032658/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1032658,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1032658/?format=api",
    "text_counter": 197,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": " Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi nichangie Hoja ya Hotuba ya Rais tunayempenda. Katika mambo yaliyonifurahisha, la kwanza ni kuhusu kupambana na ufisadi. Lau litafuatilizwa kisawa sawa, Kenya yetu itafika mbali. Nampongeza Rais kwa sababu ameleta matumaini. Awali, hungeweza kuona Waziri akienda kuhojiwa mbele ya Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC), lakini sasa hivi, tunaona Mawaziri kadhaa wakienda mbele ya tume hiyo kuhojiwa. Kwa mfano, sasa hivi, mitandaoni tunaona Waziri, Prof. Magoha akienda kwa EACC pamoja na wengine waliomtangulia kwenda. Kwa hivyo, tunampongeza Rais kwa kuleta haya matumaini. Kupitia kwa Utaratibu wa Utendaji No.2 ya 2020, Rais aliamurisha mfumo wa utendakazi na uwajibikaji wa matayarisho ya kupambana na COVID-19. Hata hivyo, mpaka sasa ni masikitiko. Tunasikia kuwa, kwa afya, bado kaunti hazijajitayarisha vilivyo. Sasa sijui kama sisi Wakenya itabidi tuwekwe fimbo jela kwa sababau mambo yameelezwa lakini watu hawayafanyi. Pesa zinapelekwa kwa magatuzi kwa matayarisho, lakini watu hawawajibiki. Tutamlaumu nani? Rais ameshatoa njia na utaratibu wa kufuatwa, lakini watu hawazifuati kisha watamlaumu Rais."
}