GET /api/v0.1/hansard/entries/1032664/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1032664,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1032664/?format=api",
    "text_counter": 203,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": " Ahsante. Pia nilipendezwa na alivyozungumzia ugonjwa wa akili. Alisema kuwa kutakuwa na hospitali za kisasa za kitaifa za kutibu ugonjwa huu. Kule kwetu Lamu, watu wengi akili zao zimeharibiwa na dawa za kulevya. Utapata vijana wadogo wamefungiwa kwa nyumba. Maskini! Ni kwa sababu akili zao zimepotea. Ikiwa kutakuwa na hospitali hizi, zitasaidia sana. Rais pia alisema kuwe na mustakabali wa kitaifa kwa watoto wetu. Watoto wetu ndio matarajio yetu. Huo ni mustakabali mzuri ikiwa utatengenezwa kutokea kwa shule za msingi. Watoto hawa watakua kwa njia nzuri na kwa maadili. Hapa Kenya, shida si sheria na pesa, shida ni roho zetu. Kila mtu huona pesa za Serikali ni za kuliwa. Tukijenga mustakabali mzuri, tutaweza kujirekebisha tukianza na watoto. Sasa hivi, wale wanaofanya mazuri ndio wanaoonekana ni The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}