GET /api/v0.1/hansard/entries/1032930/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1032930,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1032930/?format=api",
"text_counter": 194,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nandi CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Tecla Tum",
"speaker": {
"id": 913,
"legal_name": "Tum Tecla Chebet",
"slug": "tum-tecla-chebet"
},
"content": " Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono Hotuba ya Rais mchana wa leo. Rais alisema kuwa kuna changamoto nyingi katika hospitali zetu. Kweli, madaktari wamekufa. Mheshimiwa tuliyekuwa naye, Justus Murunga, ametuaga. Natoa rambirambi zangu kwa watu wa area yake. Kuna haja ya kununua masks kwa hospitali zetu. Wale wanaotuchunga tukiwa wagonjwa ni lazima walindwe vilivyo. Jana, niliona Daktari, Hon. Nyikal akitoa machozi ikanifanya nitokwe na machozi nikiwa nyumbani kwangu kwa sababu nina muheshimu. Tutilie maanani hali zao. Tuwache kila kitu na tushughulikie afya za watu wa Kenya. Rais alisema hakuna mtoto atakayewachwa nyuma, hata wale wanafunzi waliopata watoto wakiwa wadogo. Kule Nandi County, niko na wanafunzi 3,303 wenye umri kati ya miaka 14 na 19 waliopata watoto. Nawaomba walimu wakuu, kama alivyosema Rais, wasirudishe mwananfunzi yeyote aliyepata mimba nyumbani kwa sababu haikuwa shida yao kuzipata. Ni ugonjwa wa COVID-19 uliofanya watoto wakae nyumbani na wakatangamana na wenzao. Rais ametoa amri kuwa hata kama hao waschana wemezaa, warudi shuleni Januari. Kuhusu watu walio na akili isiyo timamu, Rais alisema hospitali ya Mathari National Teaching and Referral Hospital itaboreshwa. Natoa pongezi kwa hilo. Kwa sababu ya ugonjwa wa COVID-19, watu wamepoteza kazi na umaskini umeongezeka nchini. Ninajua kwamba hilo litashughulikiwa. Jana jioni tuliona mtu aliyenajisi watoto wake wawili, mmoja akiwa na umri wa siku nne na mwingine wa miaka minne. Tunataka aende kutibiwa Mathari ili watoto wetu wabaki salama. Kuhusu Building Bridges Initiative (BBI), iko sawa. Hata hivyo, hoja ya akina mama Bungeni ni lazima ishughulikiwe. Hatuwezi kutolewa wawakilishi wa akina mama 47 tupelekwe Seneti, mahali ambapo hatutaongea juu ya ugawaji na matumizi ya pesa katika nchi ya Kenya. Akina mama wa nchi hii ni lazima washughulikiwe. Hatuwezi kutolewa mahali na kutupwa kwingine. Sisi ni asilimia 52 katika nchi hii, na hoja zetu ni lazima zishughulikiwe vilivyo. Kuhusu pending bills, tuliambiwa wizara husika zitalipa. Wizara husika zilipe hizo pesa haraka. Kwa sababau ya madeni waliyonayo, Wakenya wanajiua. Wakenya wako na shida. Vijana The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}