GET /api/v0.1/hansard/entries/1032931/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1032931,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1032931/?format=api",
"text_counter": 195,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nandi CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Tecla Tum",
"speaker": {
"id": 913,
"legal_name": "Tum Tecla Chebet",
"slug": "tum-tecla-chebet"
},
"content": "wamechukua mikopo na pesa zao ziko kwa Serikali Kuu na serikali za kaunti. Nikikutana na vijana, hawana motisha . Kwa hivyo, ni muhimu Serikali zishughulikie madeni ya watu ili watu wasijiuwe. Shule zitafunguliwa Januari. Zikifunguliwa, wazazi watalipa karo na nini? Mwisho, watoto wetu wahudumiwe na wanunuliwe barakoa. Walimu wanunuliwe barakoa pia. Jana kuna mwalimu aliaga dunia na nikaona watoto wakipiga nduru. Zile pesa zote zilizoko, zitumiwe kwa kutilia maanani maisha ya Wakenya. Sisi sote tunaogopa, hatujui tutabaki wangapi itakapotimia mwaka wa 2022, inavyosemwa na kuimbwa, kama afya zetu hazitiliwi maanani. Ahsante."
}