GET /api/v0.1/hansard/entries/1032940/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1032940,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1032940/?format=api",
"text_counter": 204,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "wabaya. Kama wewe huibi na huna pesa za kupatia watu kwa matanga na kufanya mambo wanayotaka wananchi, utaonekana mbaya kwa sababu wananchi wamezoea kuwa Wabunge wote wana pesa. Kusema ukweli, labda ikiwa Mbunge ana biashara zingine, mshahara wake hautoshi kufanya haya mambo. Kwa hivyo, huu mustakabali wa Kitaifa ni muhimu. Naona muda unaisha. Rais alizungumzia elimu. Tunataka elimu iende mpaka mashinani ili, kwa mfano, kile mwananfunzi wa Nairobi atakachopata ndicho mwanafunzi wa Lamu atakachopata vile vile. Pia, alizungumzia usalama ambao ni muhimu haswa kwa sisi watu wa mipakani . Tunahitaji usalama. Tunataka ukuta umalizwe kujengwa, mipaka ifunguliwe na mikakakti iwekwe kwa sababau sisi tuna jamaa zetu upande ule mwingine na tumetenganishwa. Kuna Wabajuni Wasomali na Wabajuni Wakenya. Kuna mengi ya kuzungumza lakini wakati umeisha. Nampongeza Rais. Ahsante."
}