GET /api/v0.1/hansard/entries/1033072/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1033072,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033072/?format=api",
    "text_counter": 61,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": " Mimi ni Mbajuni. Sisi ni wale waliotengwa na bado tu wachache. Tunawahimiza watu wazaane ili tuwe wengi. Nimeamka kuunga mkono ombi la Mhe. Baya. Ni kweli hao wapendwa wanadhalilishwa hapa Kenya. Kuna mambo mengi hawapati kule Tanzania na huku Kenya pia hawapati. Si wao peke yao. Kuna tatizo zaidi kule kwenye mipaka. Mipaka ilipowekwa Lamu, iligawanya jamii. Kuna Bajuni wa Somalia na Bajuni wa Kenya. Bajuni wa Somalia wakakaa kwa maisha. Kuna babu zetu walioa kule na wa kule wakaoa Kenya. Kuna watoto walizaliwa kule na wengine wa kule wakazaliwa huku. Ni ndogo lakini imegawanywa. Kulipotokea shida Somalia na watu wakapigana, walikimbilia Kenya kutafuta hifadhi. Hao watu wako Kenya eneo la Kiunga kwa zaidi ya miaka arubaini sasa. Wengine wameolewa huko na wakazaa. Wengine huku wakazaa. Hapa sasa hawana vitambulisho vya Kenya. Kuna mmoja nakumbuka alinililia. Ana miaka karibu arubaini na alisoma Kenya akamaliza kidato cha nne. Kule kwetu Lamu ukipata C+ umepita sana. Ana C+ na hakuweza kuendelea na masomo kwa sababu hana kitambulisho. Imebidi afanye biashara pale. Kwa hivyo, hili tatizo liko. Mimi pia ombi langu litakuja kuwatetea watu wangu wa Kiunga. Ahsante, Mhe. Spika."
}