GET /api/v0.1/hansard/entries/1033079/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1033079,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033079/?format=api",
"text_counter": 68,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nairobi CWR, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Esther Passaris",
"speaker": {
"id": 12475,
"legal_name": "Esther Passaris",
"slug": "esther-passaris"
},
"content": " Mhe. Spika, nimesimama leo kumuunga mkono mwenzangu, Hon.Owen Baya, kwa hili ombi ambalo ameleta hapa Bungeni. Mimi mwenyewe ninafahamu sana watu ambao hawana ukoo nchini. Tumekaa na watu hao kwa miaka miwili tukizungumza, wakitueleza shida ambazo wanapatana nazo. Walipoona Rais akipeana vyeti vya kukaa kwa Wanamakonde, hawa wa Kibera pia waliona kuwa wana uwezo. Saa zile Washona walikuja hapa Bunge kutuletea ombi lao, walisema kuwa Rais wa kwanza, Mhe. Jomo Kenyatta, aliwatambua na kama angekuwa amebarikiwa na maisha ya mbeleni zaidi, angekuwa ameshawatimizia ombi lao la kuonekana na kujulikana kama Wakenya. Washona wenyewe walipewa shamba karibu na Chuo kikuu cha Daystar, ambako walijenga kanisa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}