GET /api/v0.1/hansard/entries/1033080/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1033080,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033080/?format=api",
"text_counter": 69,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nairobi CWR, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Esther Passaris",
"speaker": {
"id": 12475,
"legal_name": "Esther Passaris",
"slug": "esther-passaris"
},
"content": "lao. Ni watu ambao wana maombi na wanakaa na ukweli na undugu na Wakenya. Hawajui nchi nyingine. Wakoloni walipokuwa hapa, walileta watu kutoka Afrika nzima. Tuko na watu kutoka Rwanda, Zimbabwe, Pemba na Tanzania. Hao watu wote waliletwa hapa kukaa na sisi na kufanya kazi kama kujenga reli. Lakini sasa wako na shida sana. Hawatambuliwi. Tukiwa na hii Huduma Namba, watakuwa na shida zaidi. Hata kama tunataka kuwatambua kama Wakenya, ni lazima pia tuwasamehe kwa sababu kuna mambo waliyofanya, ambayo si ya haki – kama kwenda kuchukua vitambulisho ama kuwaandikisha watoto wao kuwa wamezaliwa Kenya ili waweze kwenda shule au hospitali. Kuna familia nyingine tunazozitambua ambazo watoto wao wamezaliwa huku, lakini wazazi hawatambuliki. Kuna wengine wamemaliza masomo ya O-Level lakini mpaka sasa hawawezi kujiunga na vyuo vikuu. Mhe. Spika, sisi kama Wabunge tulikuomba tuwe na caucus ya kuangalia hao watu ambao hawana jinsi ya kujulikana ama kutambulika kama Wakenya. Tuko na wengi na si community moja. Katiba yetu inasema kuwa haifai watu wengine wapate na wengine wakose. Sisi sote kama Wabunge tunajua kuwa hao watu ambao wako nchini mwetu na wameishi na sisi wanafaa watambulike kama Wakenya. Kwa hivyo, naunga mkono hilo ombi la watu wa Pemba na watu wote wengine kama vile Washona na wale wa Rwanda ambao wameishi na sisi kama Wakenya, ili watambulike kama Wakenya. Ahsante, Mh. Spika."
}