GET /api/v0.1/hansard/entries/1033082/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1033082,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033082/?format=api",
"text_counter": 71,
"type": "speech",
"speaker_name": "Baringo CWR, KANU",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Gladwell Cheruiyot",
"speaker": {
"id": 13231,
"legal_name": "Gladwell Jesire Cheruiyot",
"slug": "gladwell-jesire-cheruiyot"
},
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika, kwa nafasi hii umenipa ili niweze kuchangia ombi hili, ama tunaiita ardhihali katika kitabu chetu ambacho tumepewa kipya. Nataka kuchangia ardhihali ya yule Mheshimiwa aliyetoa Hoja kule Marsabit na kusema kwamba misitu yetu ni ya muhimu sana. Hii misitu ambayo tunataka kuhifadhi ndio maisha yetu. Tusipokuwa na miti nchini, tukiweza kujenga vyumba vikubwa, kutaka kutengeneza mambo ya siku hizi na tusahau mazingira, unapata kwamba sisi kama binadamu tutaumia. Si Kenya peke yake ila dunia mzima. Miti ni muhimu kwa sababu bila miti hakuna uhai. Hewa ambayo tunapumua inatokana na miti na ni hewa safi. Kule Baringo ambako nimetoka, shida ambayo tuko nayo ya mafuriko inatokana na mmomonyoko wa udongo. Sehemu za juu zimekatwa miti; miti ambayo ingezuia mchanga kufurika kwenye mito. Kwa sasa, watu wanaumia na hawajui sababu. Tuhifadhi misitu yetu maana ndio maisha yetu. Miti ni dawa, ndio tunatumia kupata karatasi za kuandikia, kujenga nyumba zetu, kupika na ndiyo tumekalia, kama viti. Kwa hivyo, tuhifadhi mazingira kwa sababu ni muhimu. Wale ambao wanataka kukata misitu kusudi wajenge, Kenya bado ni kubwa. North Eastern shamba ni kubwa. Baringo, kwetu, pia shamba ni kubwa. Kujeni kule mkajenge muache kukata misitu. Ahsante, Mhe. Spika."
}