GET /api/v0.1/hansard/entries/1033233/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1033233,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033233/?format=api",
"text_counter": 222,
"type": "speech",
"speaker_name": "Baringo CWR, KANU",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Gladwell Cheruiyot",
"speaker": {
"id": 13231,
"legal_name": "Gladwell Jesire Cheruiyot",
"slug": "gladwell-jesire-cheruiyot"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa nafasi hii umenipa nichangie Hoja hii. Hotuba ya Mhe. Rais ilifana kabisa. Aliongea mambo mengi ambayo sio lazima sisi sote tuyafurahie. Lakini kwangu, nasema ni asante maanake aliyataja mambo yanayoguza mwananchi wa kawaida. Janga ambalo liko kwa sasa la Korona, ama COVID-19, ni janga ambalo limeleta shida humu kwetu mpaka hata sisi tumepoteza ndugu na marafiki na watu wa karibu kwa sababu ya ugonjwa huu. Anaposema wametenga kama nchi pesa nyingi sana za kupigana na janga hili, ni kweli lakini kuna shida kwamba wale ambao wanapewa nafasi ya kuhudumia wananchi hawana utu wa kutumia fedha hizi kwa njia inayofaa. Jinsi ambavyo sisi wawakilishi wa akina mama katika nafasi zetu za Ubunge tunavyotumia fedha za NGAAF na zile za NG-CDF, na tumeelewa mikakati ya kutumia zile fedha, inafaa pia kule kwa uongozi wa ugatuzi wawekewe mikakati ili fedha ambazo tunapanga ziende huko mashinani zitumike kwa ratiba ambayo imepangwa ili wale wasiwe na njia ya kutumia fedha kwa njia ambayo wanafikiria. Ni vyema kwamba tuone fedha ambazo ziliwekwa pale, kwanza zile kila kaunti ilipewa za Korona, tujue zimefanya kazi gani ili tuone kinagaubaga kwamba fedha zile zimefanya kazi na mwananchi anafaidika. Kuna mambo mengi ambayo yaliongelewa, hata kuendeleza uchumi wa nchi hii. Ni bayana kwamba vijana wa nchi hii hawana kazi. Na katika ile hali, Mhe. Rais anasema kwamba tunahitaji kuwa na uwiano na utangamano. Watu wakae pamoja. Tuishi kwa amani na tusigawanyishwe kwa upigaji wa kura. Ndiposa anajaribu kuleta huu muungano wa marejesho ili watu wakae pamoja ndio tusikizane na nchi hii ipate amani ya kudumu. Tunajua kwamba vijana wetu hawapati kazi kwa sababu wanamaliza masomo yao kwa wingi na baada ya hiyo, hawawezi kupata kazi wote. Wengi wao ambao wamehitimu kwa masomo hawapati kazi kwa sababu nafasi za kazi nchini ni chache. Kwa hivyo, wale wanaowekeza katika nchi hii kwa biashara na mambo mengine ya kibinafsi ndio wangeweza kuajiri vijana hawa kazi. Shida ni kuwa hawa ambao wanatakiwa kuja kuwekeza katika nchi hii hawana tena imani nasi na wanaogopa kuwekeza pesa zao katika nchi hii, maanake kila baada ya miaka mitano, tuko vitani na kukikimbia. Ni vyema kwamba wamefikiria tukae pamoja. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}