GET /api/v0.1/hansard/entries/1033236/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1033236,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033236/?format=api",
"text_counter": 225,
"type": "speech",
"speaker_name": "Malindi, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Aisha Jumwa",
"speaker": {
"id": 691,
"legal_name": "Aisha Jumwa Katana",
"slug": "aisha-jumwa-katana"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwanza, nimesimama kupongeza Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Kenya aliyoitoa wiki iliyopita. Ni jukumu lake kikatiba kufika mbele ya Bunge na kutoa ratiba ya vile nchi na maendeleo ya kitaifa yanavyopaswa kuendelea na jinsi yalivyo na tunavyopaswa sisi kama taifa kuendelea Kitu ambacho kimenigusa sana ni kuhusu ile hospitali ambayo alisema hospitali ya kuangalia maswala ya akili; Hospitali ya Mathari. Na hata niseme hivi na mimi nikiwa ni shahidi wa juzi tu ya kwamba hospitali hii ama taasisi hii inahitaji kuangaliwa kwa umakini sana. Kule nje Wakenya wanaumia kwa sababu kuangaliwa akili ama kwenda kupimwa akili ni sharti moja katika mahakama zetu kabla hujaweza kushtakiwa na makosa ya jinai. Ni lazima uangaliwe kwanza akili kama ziko timamu. Nasema hivyo kwa vile mimi nilipitia hayo juzi na nimeona Wakenya wanaumia sana. Katika Mkoa wa Pwani taasisi moja peke yake ambayo ni CoastGeneral Hospital na daktari mmoja katika Pwani nzima ndiye anayesimamia maswala hayo ya kuangalia akili za wale wote walioko rumande kabla hawajashtakiwa na makosa ya mauaji. Nilisikitika sana na nikaona ya kwamba mengine Mungu anayaruhusu yafanyike ili wengine wakaweze kutetewa. Hilo swala ni jambo ambalo linawaumiza Wakenya wengi ambao hata wenzao na miili yao na maisha yao yanaisha ndani ya seli kwa sababu ya kukosa huduma muhimu kama hii. Namshukuru sana Rais na ningependekeza ya kwamba labda mbeleni kabla kipindi chetu hakijaisha tutakuwa na sheria ambayo labda mimi mwenyewe kama mhusika mkuu nitakuwa nimeileta kuhakikisha ya kwamba hospitali hizi hazibaki Nairobi tu lakini kila kaunti kuwe na hospitali hii ambayo itakuwa ni muhimu sana katika maswala ya kuweza kunusuru wengi ambao labda wako pale kwa maonevu lakini wamewekwa pale kwa sababu ya kukosa huduma hii muhimu. Pia vile vile, katika swala hilo ni kwamba ikiwa leo ni siku ya wanaume katika dunia, nataka niseme ya kwamba wanaume wengi wanateseka. Unaeza kuwaona wako hivi wanacheka lakini kwenye majumba yao wanapitana na mashaka. Akili zao sio vile tunavyofikiria ziko sawa. Tumeona kisa hapa leo Nairobi Women Hospital ambapo mtoto wa miaka minne na mtoto wa siku nne amenajisiwa na babake. Huyo ni mtu ambaye kweli ana akili timamu? Tunaeza kuwa tunacheka nao lakini akili zao si nzuri. Akili zao lazima ziboreshwe, Kaimu Bi. Kaimu Spika wa Muda. Jambo lingine ambalo nataka kusema ni kwamba Kiswahili - na nataka nipongeze, though haikuwa kwenye hotuba ya Rais lakini alituzindulia - katika Bunge hili, Kiswahili kitukuzwe na kizungumzwe kwa sababu sisi tunatafuta kura kule chini kabla kuja hapa Bungeni kwa lugha labda tatu, ya mama, ya taifa ambayo ni Kiswahili, lakini tukifika hapa, tunaunda sheria katika lugha moja tu ya Kiingereza. Huwa tunawaundia sheria kule lakini hawatuelewi. So, iwe Bungeni Kiswahili kitukuzwe mpaka kortini kwa sababu kule haki zinatafutwa na lugha ambayo wananchi wengi hawaielewi. Na mwisho ni kwamba COVID-19 imetufunza mengi. Juzi tulipoteza ndugu wetu hapa. Na ni kwa sababu gani sisi wenyewe kama Wabunge hatuangalii hata hospitali zetu kule mashinani ziko vipi? Sisi Wabunge tuna medical cover nzito nzito wakati wananchi hawana cover. Wabunge The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}