GET /api/v0.1/hansard/entries/1033239/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1033239,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033239/?format=api",
    "text_counter": 228,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taita Taveta CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Haika Mizighi",
    "speaker": {
        "id": 13274,
        "legal_name": "Lydia Haika Mnene Mizighi",
        "slug": "lydia-haika-mnene-mizighi"
    },
    "content": " Shukrani sana, Naibu Spika wa Muda. Nakushukuru kwa kunipa fursa ili niweze kuchangia swala hili ambalo tunaliongea hapa na ni swala kuhusu Hotuba ya Rais. Ninataka kusema ya kwamba Hotuba ya Rais ilikuwa sawa. Kuna mambo mengi ambayo aliyataja na mojawapo ikiwa ni janga hili la Coronavirus. Mimi nataka kusema hivi: Coronavirus ipo, Coronavirus imeuwa, Coronavirus imeumiza na inazidi kuumiza Wakenya. Wakenya wanakufa, madaktari wanakufa, na hata sasa Wabunge na walimu wanakufa. Ni uchungu sana kuona kwamba madaktari ambao tunawategemea kutusaidia wakati huu mgumu hata wao pia wanafariki kwa ajili ya ugonjwa huu. Watu wanaumia mioyo. Watu wanaumia akili. Watu wana uoga mkubwa sana. Ni wakati sasa kama nchi wa kuwajibika bila samahani. Ni wakati wa kuona kwamba hospitali zetu tumeweza kuziboresha kila sehemu ya nchi hii. Swala lingine pia ambalo ningependa kulitaja ambalo lilikuwa kwa Hotuba ya Rais ni jambo la elimu. Nashukuru kwa sababu kulikuwa na maswali mengi ya kwamba watoto wamekaa nyumbani muda mrefu na kunakuwa na sintofahamu ya kuwa ni lini basi watoto hao watarudi shuleni ama itakuwa namna gani kuhusu maswala yetu ya elimu. Napongeza Idara ya Elimu kwa sababu walitoa tarehe ambazo shule zetu zitafunguliwa. Swala kuu kwa wakati huu ni je, tumeweka miundo misingi ya kuweza kuwakaribisha watoto wetu ama kuweza kuwarudisha watoto wetu shuleni? Tunayo madarasa ya kutosha? Tunayo madawati? Na je, ile ada ya shule itakayolipwa tuko nayo? Tunajua wananchi wengi wamekuwa nyumbani na wengi wamekosa kazi kwa sababu ya hii mambo ya Coronavirus. Hili ni janga. Na hawana fedha sasa. Je, watalipa vipi hiyo ada? Tunajua watoto wetu wamekaa nyumbani na wamekuwa wakubwa na hata zile sare zao za shule haziwatoshi sasa. Kwa hivyo, itakuwa ni kama mwanzo mpya kupeleka watoto kuanzia sare ya shule, kuanzia vitabu na hata ada za shule. Kwa hivyo, ni wakati wa kuweza kuangalia hilo swala na kuona ni vipi tutasaidiana na kusaidia jamii itakapofikia kurudisha watoto wetu shuleni. Nikimalizia pia, swala lingine ambalo Rais alitaja ni mambo ya BBI. Kuhusu BBI nitasema kama kina mama bado tunahisi tumenyanyaswa na tunasema bado kuwe na muda wa majadiliano. Hii si kwa sababu ya akina mama peke yao, ila wadau mbali mbali waweze kuja na kutoa hoja zao pale ili kuwepo na uwiano. Nasema asante sana. Nikimalizia, pia niwapongeze kina baba wote walioko hapa na niwapongeze pia kina baba manyumbani na kina baba wote wa Kenya wale wanatenda wema kwa sababu leo ni siku ya kina baba; International Men's Day. Asante sana, kwa kunipatia hii fursa."
}