GET /api/v0.1/hansard/entries/1033249/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1033249,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033249/?format=api",
    "text_counter": 238,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": " Asante sana, Naibu Mhe. Spika Wa Muda. Mimi pia napata nafasi hii kuweza kuzungumzia Hotuba ya Mheshimiwa Rais na niseme ilikuwa ya kizalendo sana. Alizungumzia mambo mengi sana. Nimeskia Waheshimiwa wenzangu wakizungumzia janga la Corona. Jamani hakuna ambaye hakumwona Mheshimiwa Rais aking’ang’ana wakati tulipata kesi ya kwanza ya Corona. Hata viongozi wengine tukiwemo sisi wenyewe tulisema ya kwamba Corona ni uongo na ni jambo la kutengenezea watu pesa na ni mambo ya propaganda . Kwa hivyo, mimi nataka niseme kuwa wakati tunazungumzia ufisadi katika mambo ya Corona, sisi Wabunge tuna jukumu la kuangazia mambo ambayo yalifanyika katika taifa letu la Kenya. Hata Bunge la Seneti lina nguvu ya kuangalia mambo ya afya katika kaunti zetu. Afya imegatuliwa na iko mashinani. Ningetaka kumwambia Mhe. Rais katika juhudi zake alizofanya kupigana na janga hili, aongeze nguvu zaidi ili tuweze kupata vifaa na wahudumu wa afya zaidi na bima ya afya ya kitaifa ya kuweza kuangalia Wakenya kwa sababu ya janga hili."
}