GET /api/v0.1/hansard/entries/1033253/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1033253,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033253/?format=api",
    "text_counter": 242,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Pia, Mhe. Rais alizungumzia ule mpango wa mambo ya boda boda. Hii ni njia moja ambayo itaweza kujenga ajira zaidi kwa vijana wetu kule nyanjani. Basi mpango kama huu uweze kusambaswa kule mashinani katika maeneo Bunge yetu na kauti zetu ili kujenga ajira. Mhe. Raisi alisema kuwa vijana wajitokeze ili waweze kupate mshahara na kuwa wamiliki wa fedha. Kwa hivyo, ni lazima wajenge uwezo katika kupata zabuni kama za madeski, za kufanya kazi ya kuleta vifaa vya kupigana na Corona na za ule mpango wa kutengeneza nyumba za kisasa katika makazi duni. Hii ni kwa sababu tunataka kuweka Wakenya katika hali nzuri. Mhe. Rais pia alizungumzia mambo ya mkusanyiko wa digiti au ditigisation ya mambo ya mashamba ama ardhi. Mimi ni mwanakamati wa Kamati ya Ardhi na tumeweza kutenga pesa na sasa hivi kuna kaunti ambazo tayari wameweza kuitumia. Kwa hivyo, namuunga mkono Mhe. Rais kwa jambo kama hili. Pia, mambo ya mafunzo ya vijana, kuongeza madarasa, madawati, vifaa na waalimu ili ule mpito wa watoto kusoma kutoka shule ya msingi hadi shule ya upili uweze kupatikana ndiposa watoto wetu waweze kuwa na elimu. Mhe. Rais alivyozungumzia kuhusu watoto kurudi shuleni kufikia Januari mwaka ujao, alisema kuwa mikakati iwekwe ili wazazi wasihangaishwe na mambo ya karo. Janga la Corona limerudisha nyuma uchumi wetu. Wazazi wapewe nafasi waweze kulipa kwa njia watakayoweza ili kusomesha watoto wao. Naunga mkono Mhe. Rais kwa mambo ambayo amefanya kama kutengeneza magari hapa Kenya. Yamekuwa assembled hapa na vijana walipata ajira. Pia, mambo mengine kama kuweze kujenga viwanda katika taifa letu la Kenya kama sampuli iliyofanyika ili watoto wetu waweze kupata ajira."
}