GET /api/v0.1/hansard/entries/1033262/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1033262,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033262/?format=api",
"text_counter": 251,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi South, ODM",
"speaker_title": "Hon. Ken Chonga",
"speaker": {
"id": 13374,
"legal_name": "Richard Ken Chonga Kiti",
"slug": "richard-ken-chonga-kiti"
},
"content": "Pia, tuko na kesi ambazo watu zaidi ya miaka 100 wamezaana na kuzikana pale. Watu wamefanya ukuzaji wa mimea tofauti na nafaka ambazo zinawakimu kimaisha kwa sababu zikishapelekwa sokoni ndio nao wanapata chochote cha kuwasaidia. Lakini unapata ghafla bin vuu asubuhi moja mtu amekuja anasema lazima mvunje na muhame. Visa kama hivi ndani ya Kilifi Kusini vimejaa. Si Shariani, si Mtepeni, si Vipingo, si Shimo la Tewa, kila uchao visa hivi vimejaa. Hivyo basi, ninaunga mkono kikamilifu Hotuba hii nikitumaini kwamba yale yaliyozungumzwa na Rais yatapata mwelekeo mwafaka na matatizo haya ambayo yanatukumba ya mashamba yatapata suluhu ya kudumu. Nasema hivyo kwa sababu niko na wasiwasi na tashwishi. Wewe na mimi tunakumbuka kwamba kuna tume nyingi sana ambazo ziliundwa kuchunguza kuhusu masuala ya dhuluma ya mashamba ikiwemo tume ya Ndung’u. Ninajua mambo kama haya yako katika ripoti ya tume ya Ndung’u lakini kufika sasa imekuwa ni ndoto tu maana haijabainika wazi ni lini ukweli ambao uko ndani ya ripoti ile utaletwa nje watu wajue nini ambacho kimefanyika na mwelekeo ni gani. Hivyo basi, isiwe tu kwamba hili suala lilitajwa. Tunaomba kwa hisani ikiwezekana pia tuhakikishe tunaona mambo yakifanyika. Kabla muda wangu haujaisha, niko na suala lingine ambalo ninataka kuligusia kwa juu sana. Ni kuhusu bima ya kitaifa. Tunajua kwamba tuko na bima ya kitaifa lakini watu wengi hawana uwezo, hususan wazee. Ningeomba wazee ambao wako rika la miaka 70 kuendelea wapewe huduma hii bure katika hospitali zote. Saa hii tuko na janga la Corona. Wengi wanaoathirika ni hawa. Tunaomba hili pia ni suala ambalo linafaa kuangaliwa kwa kina wazee wetu waweze kuchungwa. Nitamalizia na suala la ufisadi. Kenya ni maskini kwa sababu ya ufisadi. Kila uchao utapata kesi za ufisadi. Nafikiri imefika wakati hizi sheria za Bunge ziweze kuundwa upya ilimradi ziweze kuhakikisha kwamba watu hawatajihusisha na visa vya ufisadi. Tunasema vijana hawana kazi na viwanda haviwezi kufufuliwa lakini kila uchao unasikia mabilioni ya pesa yamepotea."
}