GET /api/v0.1/hansard/entries/1033297/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1033297,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033297/?format=api",
"text_counter": 286,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nominated, FORD-K",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Nasri Ibrahim",
"speaker": {
"id": 13173,
"legal_name": "Nasri Sahal Ibrahim",
"slug": "nasri-sahal-ibrahim"
},
"content": "(NG-CDF). Hatusemi kuwa ni NG-CDF pekee itatumika. Tunataka Serikali kuu nayo isaidie ujenzi wa madarasa. Na si madarasa pekee. Madarasa yatakayojengwa yawe ya maana na yahudumu kwa miaka mingi sana. Mtoto ataweza kusoma na kuelewa vizuri ikiwa darasa ni nzuri na ana mahali pa kuketi. Hiyo ni muhimu sana. Kwa afya ya akili, Rais alisema kuwa atajenga hospitali kubwa sana. Tunakaribisha hiyo na kufurahia kwa sababu watu wengi hapa nchini wana matatizo ya kiakili na hawajijui. Wengine wanasumbua watoto na wake wao. Wengine wako barabarani. Hospitali hizi zikijengwa zitasaidia. Madaktari wengi wataenda kwa chuo hicho wajifunze vile watahudumia watu ambao wana magonjwa ya akili. Jambo lingine nataka kuzungumzia ni uchumi. Uchumi wetu ni mbaya sana. Hatuna kitu cha kujivunia. Nasema hivyo kwa sababu mimi ni mwanabiashara. Biashara iko chini sana. Hali hiyo imeletwa kwa ajili ya ugonjwa huu wa COVID-19. Ukienda kwa maduka, hakuna mtu anayenunua kwa sababu watu wengi wamepoteza kazi zao. Wakenya wengi hawana kazi kwa sababu ya COVID-19. Tumekataa wale ambao wanatufanyia kazi kwa nyumba zetu waje kwa sababu ya ugonjwa huu wa COVID-19. Kama hawana pesa, nani atawasaidia kununua vitu kwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}