GET /api/v0.1/hansard/entries/1033298/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1033298,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033298/?format=api",
"text_counter": 287,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nominated, FORD-K",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Nasri Ibrahim",
"speaker": {
"id": 13173,
"legal_name": "Nasri Sahal Ibrahim",
"slug": "nasri-sahal-ibrahim"
},
"content": "maduka? Hiyo imeleta shida. Tunataka Serikali ichukue hatua ya dharura kuwapa wafanyibiashara mikopo ili wajisaidie wenyewe. Kuhusu ajira, kuna shida. Vijana wengi Kenya hii hawana kazi. Hatuwezi kujivunia na kusema tumeajiri watu wa mkono kwa barabara au kwa reli. Lakini vijana ambao ni wasomi wako na shida. Juzi nimesikitika kuona kwa televisheni vijana ambao walimaliza chuo kikuu na hawana kazi. Mmoja anauza samosa, mwingine anapanda miti, mwingine anatengeneza manure, mwingine anarandaranda bado anatafuta kazi, mwingine ni engineer na anabeba mawe na mchanga. Hivyo si vizuri. Tunaharibu vijana wetu. Ndio maana vijana wengine wanaenda kwa Al Shabaab. Hawana kazi. Hakuna kitu cha kujivunia hapa. Vijana wanateseka. Wanarandaranda kwa mitaa na hiyo haisaidii nchi yetu. Mwishowe, nataka kutuma risala za rambirambi kwa familia ya Mheshimiwa Murunga. Tunasikitika na kumwomba Mungu ampeleke mahali pema peponi."
}