GET /api/v0.1/hansard/entries/1033300/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1033300,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033300/?format=api",
    "text_counter": 289,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Tana River CWR, MCCP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Rehema Hassan",
    "speaker": {
        "id": 13275,
        "legal_name": "Rehema Hassan",
        "slug": "rehema-hassan"
    },
    "content": " Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii nichangie Hotuba ya Rais. Haikuwa mbaya, ilikuwa hotuba nzuri. Lakini kuna yale yaliyonivutia kutokana na hiyo Hotuba. La kwanza ni swala la ufisadi. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa sababu anang’ang’ana sana kupigana na ufisadi. Lakini wale wanaomwakilisha kutekeleza masuala ya ufisadi hawawajibiki vilivyo. Naona wamechukua mikondo ya siasa. Huwa watu wanafuatiliwa kwa mirengo. Naona siasa zimeanza mapema. Kama wewe si wa mrengo fulani, basi wewe ndio utaandamwa. Lakini kama wewe ni wa mrengo fulani, basi uko huru kufanya utakavyo. Kwa hivyo, naomba wahusika wamuunge mkono Mheshimiwa Rais kupigana na ufisadi bila ubaguzi. Mfisadi ni mfisadi. Hana ukubwa wala udogo. Suala lingine ni kuhusu maendeleo yale ametufanyia, haswa kwa masuala ya barabara. Tumeona anawajibika sana. Huzuni yangu ni kuwa naona barabara nzuri katika miji mikuu ndizo zinaangaliwa zaidi. Huko barabara zaongezwa zikiongezwa. Kuna sehemu ambazo hali ya usafiri iko na shida mpaka sasa."
}