GET /api/v0.1/hansard/entries/1033304/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1033304,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033304/?format=api",
"text_counter": 293,
"type": "speech",
"speaker_name": "Tana River CWR, MCCP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Rehema Hassan",
"speaker": {
"id": 13275,
"legal_name": "Rehema Hassan",
"slug": "rehema-hassan"
},
"content": "Ninataka kuzungumzia suala la BBI. Siyo hoja mbaya kurekebisha Katiba. Tangu mwanzo, wakati Katiba ya 2010 ililetwa, tayari ilikuwa na matatizo. Watu walilalamika na wakasema ilikuwa na shida. Wakasema tuipitishe halafu tutarekebisha. Watu wanalalamika. Wanasema kuna matatizo katika Ripoti ya BBI. Wacheni tusuluhishe ndiyo tuepuke kurekebisha Katiba mara kwa mara. Tusipitishe halafu tuje turekebishe tena. Turekebishe sasa. Pia, haina haja ya kupoteza pesa. Hili ni suala la sisi, Wakenya. Tunaweza kukaa tujadiliane na pesa hizo ziende kwa maendeleo mengine."
}