HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1033323,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033323/?format=api",
"text_counter": 312,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kasarani, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mercy Wanjiku",
"speaker": {
"id": 13364,
"legal_name": "Mercy Wanjiku Gakuya",
"slug": "mercy-wanjiku-gakuya-2"
},
"content": "Na mimi kama Kiongozi wa hapa Nairobi, kuna mambo mengi aliyozungumzia ambayo yalinigusa. Haswa, alivitaja vyeti miliki ambavyo vimepeanwa kwetu. Tumeweza kusaidika na shilingi bilioni sita ambapo wakazi kama 40,000 walipata vyeti miliki vya ardhi na bado vingine vinaendelea kupeanwa. Lakini kunazo changamoto kwa sababu kwa vyeti hivyo, kuna ile mizozo ya ardhi zaidi ya 5,000 ambayo mpaka sasa haijaweza kutatuliwa. Hata kama huwa tunahakikisha kuwa kila mtu amepata haki, hivi karibuni lazima watu watapata haki. Kwa mfano, katika eneo Bunge langu la Kasarani, sio tu waliopata vyeti hivo, tunao watu ambao wamekaa katika mashamba ya wenyewe. Vile vile, katika Agenda Nne Kubwa za Rais Uhuru Kenyatta, Serikali inahakikisha kuwa watu wamemiliki nyumba. Huu ni wakati wa watu waliopewa kazi hiyo, hamna haja ya kununua mashamba sehemu zingine ndio wajenge nyumba za kufana. Miaka imepita na wananchi huenda ikawa walijenga sehemu hizi baada ya mwongozo mbaya wa wakati huo katika eneo la mashariki mwa Nairobi.Watu hawa ni wengi; hizi ni zaidi ya familia 300,000 ambazo ziko huko. Kwa hivyo, namuunga Rais mkono na tunapoendelea kupatiana vyeti hivi vya ardhi, tuweze kukumbuka familia hizi. Sheria ambazo zipo zimetosha kuhakikisha kwamba kila mtu ametosheka. Tukiangazia mambo ya chakula, chakula ni kitu muhimu. Imefika mahali katika nchi yetu ambapo hatutakuwa na hali ya kujimudu kimaisha kupitia chakula. Bila kufanya kazi na Serikali kushikilia ile mikakati ifaayo ili kuleta chakula, hakuna vile tutakavyo endelea. Tunaweza kuwa na barabara nzuri, teknolojia nzuri na maendeleo mazuri, lakini, ikiwa haya yote hayawezi kuweka chakula mezani, itakuwa ni bure kabisa. Tunapozingatia mambo ya uchumi, uchumi bora huletwa wananchi wanapopewa nafasi ya kufanya kazi. Walakini, mahali imefikia hapa Kenya, kila mtu akimaliza shule, akienda kuomba mkopo kwa Serikali, anaulizwa ni biashara gani anataka. Swali langu ni: Je, iko haja gani ya kwenda kusomea masomo mengine? Basi, si tuweke masomo ya biashara kutoka shule zetu za upili hadi vyuo vikuu. Tunapowambia watu kufanya biashara, tunawafunza wizi. Hii ni kwa sababu, biashara unaweza kuifanya haraka na upate mali nyingi. Basi wanaona hakuna haja ya kwenda pole pole. Kwa hivyo, watu wale, wamefanywa na Serikali kutokuwa wanabiashara bali wanaleta miradi ambayo inawafanya watajirike haraka. Asante, Naibu Spika wa Muda, na tushikilie Rais ili kuwezesha mikakati yake kutendeka."
}