GET /api/v0.1/hansard/entries/1033356/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1033356,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033356/?format=api",
    "text_counter": 345,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kapenguria, JP",
    "speaker_title": "Hon. Samuel Moroto",
    "speaker": {
        "id": 318,
        "legal_name": "Samuel Chumel Moroto",
        "slug": "samuel-moroto"
    },
    "content": " Asante sana, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili pia nichangie mambo ambayo Mhe. Rais alisema hapa juzi akiongelesha taifa nzima. Imekuwa kawaida kwa sababu iko katika mpango wa kila mwaka ili Rias aje kutoa hotuba ya hali ya taifa katika Bunge. Itakuwa mwaka ujao tena atakapokuja kutoa hotuba ya hali ya taifa kama alivyofanya juzi na miaka iliyopita. Hii si mara ya kwanza. Hata marais wengine walifanya hivyo. Hata wakati ‘Nyayo’ alipokuwa Rais, alikuwa anakuja kutuhutubia na anapomaliza, tulikuwa tunajadili hotuba yake kwa siku saba na inabaki hivyo. Rais Kibaki pia alikuja na kusema yake. Sasa ni wakati wa rafiki na kiongozi wetu Rais Uhuru Kenyatta. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}