GET /api/v0.1/hansard/entries/1033357/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1033357,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033357/?format=api",
    "text_counter": 346,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kapenguria, JP",
    "speaker_title": "Hon. Samuel Moroto",
    "speaker": {
        "id": 318,
        "legal_name": "Samuel Chumel Moroto",
        "slug": "samuel-moroto"
    },
    "content": "Wakati Rais anakuja kuongelesha taifa, kuna mambo ambayo amepanga na yako katika moyo wake ya kwamba haya ni lazima yafanyike lakini wale watekelezaji, wale wanamsaidia wanampotosha. Kumbuka ni yeye aliweka hawa watu. Kama ni Mawaziri, ni yeye alipendekeza. Ilipofika hapa tulisema hatuwezi tukapinga kile Rais ameleta kwa sababu huenda ikawa hawa ndio wako na moyo wa kutaka kusaidia Mheshimiwa Rais kutekeleza ile mipango ameweka hapo mbele. Umesikia wakati mwingi tukizungumzia ile Miradi Nne Kuu katika jamhuri hii. Ni ile ambayo inagusa mwananchi wa kawaida. Kama hiyo ingetekelezwa, sisi hapa hatungekuwa na maneno. Nimesema kwamba Rais, kwa sababu namjua hata vile alikuwa akitembea akiwa kijana kabla hajapata kazi, ni mtu alikuwa anakula na watu na kuzungumza na watu. Anaelewa yale mateso watu wako nayo. Tukiongea kuhusu huu ugonjwa ambao uko mbele yetu, unamaliza watu tukiona. Jana hata yule alikuwa director wa medical services, Mhe. Nyikal, alilia. Yeye anaelewa kwa sababu anatoka kule. Mheshimiwa Murunga ambaye ametuwacha, hangekufa kama angepata oxygen katika ile hospitali ambayo alifikishwa kwanza. O xygen tu peke yake ya kurudisha hewa na hali ya kupumua ilisemekana ilikosekana. Hata mpaka sasa hakuna hatua Serikali imechukulia ile hospitali. Tunajua ya kwamba kuna pesa ilipeanwa. Nimesema hili Bunge lisiposaidia Mhe. Rais, tutakuwa tunamlaumu bure, lakini yuko na moyo wa kutaka kutengeneza kile kitu. Lakini mpaka saa hii hakuna mtu amechukuliwa hatua na mtu ameenda. Si huyo peke yake, bali na wengine kama vile wenzangu walisema tukiwa hapa. Kuna Wakenya, hata mahali natoka kule Kapenguria. Hospitali ya Kapenguria ni kubwa lakini utapata ya kwamba mtu akiwa mgonjwa anakimbizwa mbio mpaka Eldoret, Moi Teaching and Referral Hospital. Kwanza anapita Kapenguria na Kitale, bali pesa imepeanwa kila mahali. Kwa hivyo, ndio nataka kusema kwamba wale ambao wanahusika, especially ile"
}