GET /api/v0.1/hansard/entries/1033359/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1033359,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033359/?format=api",
"text_counter": 348,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kapenguria, JP",
"speaker_title": "Hon. Samuel Moroto",
"speaker": {
"id": 318,
"legal_name": "Samuel Chumel Moroto",
"slug": "samuel-moroto"
},
"content": "ambayo inasaidia mambo ya health, tunataka wachukue hatua. Kama mtu hawezi akafanya pale hata afadhali ajiuzulu na mwingine aje afanye, yule ambaye atakuja kusaidia wananchi. Sisi kama wafugaji tumeona ya kwamba hiki kitu ambacho mnasukuma, mambo ya BBI, tangu hii Equalisation Fund ilipoletwa ilifanya kazi mara moja na ikakufa mpaka saa hii. Mahali mimi natoka, umesikia hata leo hapo Kapedo na juzi viongozi kama yule Regional Commissioner wa Rift Valley na viongozi Waturkana,Wapokot na wa Baringo, walikuwa wanafanya mkutano lakini mpaka leo watu wanakufa baada ya wao kutoka huko. Hakuna yule amerudi kuona ni nini imefanyika mpaka sasa kwa sababu tunazungumza na wale watu wa huko. Kwa hivyo, ndio tunasema kwamba nikiwa mtu ambaye nimekaa hapa kwa muda mrefu, nataka tuangalie hili Bunge liamke na lifanye kazi yake, ili lisaidie Mhe. Rais. Nina imani na yeye kwa sababu naelewa vile alianza hadi wakati huu. Lakini wale wanamsaidia ndio wanammaliza kabisa. Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}