GET /api/v0.1/hansard/entries/1033372/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1033372,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033372/?format=api",
"text_counter": 361,
"type": "speech",
"speaker_name": "Gatanga, JP",
"speaker_title": "Hon. Joseph Nduati",
"speaker": {
"id": 13338,
"legal_name": "Joseph Nduati Ngugi",
"slug": "joseph-nduati-ngugi-2"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili niongee kuhusu Hotuba ya Rais. Ningependa nichukue nafasi hii kumshukuru Rais kwa Hotuba nzuri aliyotupa wiki jana. Yale maneno Rais aliongea yalikuwa muhimu. Alitaja tiba katika hospitali zetu, maendeleo, biashara na ajira kwa vijana wetu. Nikigusia yale aliyoyataja Rais, kwanza ni maneno ya barabara. Nachukua nafasi hii kumshukuru Rais sana maana pale kwetu Gatanga, Rais Uhuru Kenyatta ametutengenezea barabara nyingi. Gatanga ni sehemu moja ya Kenya ambayo waweza kutembea wadi zote sita kwa kuendesha gari lako kwa lami. Kwa hivyo, hili laonyesha kwamba, kwa maendeleo, Rais ametuangalia vilivyo. Barabara hizi zimetusaidia sana. Kwa kuwa Gatanga ni karibu na Nairobi, sasa tunaona watu kutoka Nairobi wakiishi Gatanga. Na ningependa niulize Rais, badala Serikali ijengee watu nyumba, Serikali itujengee barabara na wananchi wenyewe watajijengea nyumba. Jambo lingine, ninashukuru Rais kwa kutushikanisha na watu wa Nyandarua. Barabara inayotoka pale kwetu Gatanga hadi Njabini itatusaidia sana, maana itafanya biashara ikuwe rahisi. Kwetu tunakuza avocado, ngwaci na mimea mingine. Tutaweza kuenda Nyandarua na tulete viazi na karoti. Biashara itakuwa vizuri. Jambo lingine ningependa kutaja ni ugonjwa wa COVID-19. Hii wiki nimekuwa na shida sana. Leo nimetoka mazishi ya mtu ameuawa na huu ugonjwa. Jana nilikuwa na mazishi mengine na kesho pia nitaenda kwa mazishi. Pia nilienda katika shule moja pale kwetu na nikashangaa sana, maana nilipata watoto wote wamevaa barakoa vile Serikali inasema lakini katika chumba cha walimu hakuna hata mwalimu mmoja alikuwa na barakoa. Nikashangaa sana. Nikasema kama tunataka kueleza wanafunzi vile wanafaa kufanya na walimu wenyewe hawavai barakoa, itakuwa vipi? Kwa vile huu ugonjwa utaendelea, lazima kama nchi tukae chini tuone vile tutaelimisha wananchi, maana pale nyumbani hata ukiongelesha wananchi kama kiongozi na uwaambie wavae barakoa, wanakuangalia vibaya; hawaelewi chenye unasema. Kwa hivyo, lazima Serikali ijitolee, tufunze watu na tuone vile tutaendelea. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}