GET /api/v0.1/hansard/entries/1033373/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1033373,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033373/?format=api",
    "text_counter": 362,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Gatanga, JP",
    "speaker_title": "Hon. Joseph Nduati",
    "speaker": {
        "id": 13338,
        "legal_name": "Joseph Nduati Ngugi",
        "slug": "joseph-nduati-ngugi-2"
    },
    "content": "Hata watu wakishikwa wapelekwe katika korokoroni za polisi, kuko ni shida. Katika kaunti nzima, hakuna nyumba nzuri. Zile nyumba za polisi tuko nazo ni zile za zamani sana. Hata ukishika mtu na umweke pale, ugonjwa utaenea tu. Shida ingine tuko nayo kama kaunti na hasa katika Gatanga ni shida ya maji. Yale maji mnaoga nayo hapa Nairobi yanatoka kwetu lakini shule ya msingi ya Ndakaini hamna maji. Hao watoto wetu hawana maji. Katika Gatanga tunajaribu, lakini bado tuko na shida ya maji. Kwa hivyo, ningependa kuuliza Serikali na magavana wetu watusaidie ili wanafunzi wetu wakuwe na maji maana bila maji ugonjwa utaendelea kuenea na hatutaweza kuumaliza. Jambo lingine ni biashara. Tuko na vijana na tunasema hawana ajira. Ile shida tuko nayo ni vijana wetu wanakataa kuenda zile shule za ujuzi wa kazi ya mkono. Hapo ndio shida ipo. Serikali imetoa pesa nyingi, lakini vijana wetu wanadharau kazi za mkono. Na hapo ndio kazi ziko. Ile Bajeti tunapitisha hapa, pesa nyingi tunapeleka kujenga hosipitali na kuweka stima. Kwa hivyo, ningeomba vijana wetu kuwa kazi za tai zimeisha na wakubali wafanye kazi za mkono. Hata ile kazi NG-CDF inafanya ni kujenga madarasa."
}