GET /api/v0.1/hansard/entries/1033375/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1033375,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033375/?format=api",
    "text_counter": 364,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Igembe South, Independent",
    "speaker_title": "Hon. John Paul Mwirigi",
    "speaker": {
        "id": 1574,
        "legal_name": "Cyprian Kubai Iringo",
        "slug": "cyprian-kubai-iringo"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuchangia Hotuba ya Rais. Hotuba hiyo ilikuwa na mambo mengi mazuri ambayo yanafaidi mwananchi wa taifa hili. Kila wakati Rais akisimama kunena, huwa ako na mambo mazuri ambayo yanafaa kumfaidi mwananchi wa taifa hili, lakini shida ni moja tu kwa wale ambao wanafaa kuhakikisha ya kwamba yale ambayo Rais ameyaangazia yametekelezwa. Ni kweli Rais alizungumzia mambo yanayohusu vijana na ajira kwa vijana na kwamba vijana ndiyo watakuwa wenye kazi. Na aliweza kusema katika kandarasi ambazo zitakuwa zikipeanwa katika taifa hili kuwa ule ujenzi katika ile ajenda zake nne, wale ambao watakuwa wanapata zile kandarasi ni vijana lakini haya mambo saa zingine huandikwa tu. Na wale wanaofaa kuifanya kazi hii kumsaidia Rais ili aweze kuafikia yale ambayo ameweza kuyasema hawayafanyi. Ndiposa waona kama mwezi wa pili lile jambo ambalo lilifanyika ya kwamba kampuni inafunguliwa kwa mwezi mmoja na mwezi unaofuata ile kampuni inapewa kazi ya kufanya bila kuhusisha wale vijana wasio na kazi kwa sasa. Pia, wakati huu taifa hili linapitia janga la virusi vya Corona. Ni matumaini yangu kuona ya kwamba hili janga litachukuliwa kwa uzito kwa sababu wakati huu ni wakati muhimu ambapo tunafaa kuangazia ya kwamba hospitali zetu zina dawa za kutosha na vile vile maisha ya wananchi wa taifa hili yanafaa kuangaziwa sana. Hii ni kwa sababu kama taifa halitakuwa na mtu kama wananchi watakuwa wameaga dunia, sidhani kama kuna kiongozi atakayekuwa na watu wa kuongoza. Kwa hivyo, ni vyema sana wakati huu ambapo nchi inapitia hali hii ngumu, yale mambo mengine yanayoweza kufanywa baadaye yawekwe pembeni na hili jambo la ugonjwa liangaziwe sana. Hii ni kwa sababu wananchi wanapitia huu ugonjwa na kuna pesa ambazo ziko. Kwa hivyo, sio wakati ambapo Serikali inafaa kusema ya kwamba haina pesa za matibabu. Rais aliweza kuzungumzia kuhusu shule zetu na ile miradi ambayo inafaa kufanywa kule ili mwaka ujao shule ziweze kufunguliwa. Sijui kama shule zitaweza kufunguliwa kwa sababu mpaka sasa pesa ambazo tunafaa kupewa za NG-CDF bado hazijafika na bado tunatarajiwa kujenga shule. Na pia zile pesa ambazo Wizara ya Elimu inafaa kuzitoa sijui ni kwa nini wakati mwingine hawaangazii yale ambayo ni muhimu kwa sasa. Hii ni kwa sababu watoto wengi wanaaga dunia. Pia Rais aliweza kukumbuka vijana na akaweza kusema sana sana ile sekta ya boda boda ile pesa ambayo hukusanywa ni zaidi ya Ksh357 milioni. Hii ni kumaanisha watu hawa hufanya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}