GET /api/v0.1/hansard/entries/1033546/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1033546,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033546/?format=api",
"text_counter": 163,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. KFS ni kiungo muhimu sana cha kuweza kusafirisha watu wanaoishi katika maeneo ya pande mbili za Kaunti za Kwale na Mombasa. Vile vile, ni kiungo kimoja pekee kinachoweza kusaidia watu wa biashara kupita na bidhaa zao. Bw. Spika, ni jambo la kusikitisha kuona kwamba kuna njama na mipangilio inafanywa kupitia Wizara ya Uchukuzi. Wana haja ya kutoa mamlaka yote ya KFS ili iwekwe pamoja na KPA, kiwe kiungo kimoja. KPA watakuwa na mamlaka ya kuifanya KFS badala ya kuwa na mamlaka yake tofauti, iwe kitu kimoja na iwe chini ya KPA. Sisi tunapinga mipango kama hii ambayo inafanywa kisirisiri bila kuhusisha wanaotumia feri hizo. Kazi inayofanya na KFS inaweza kufanywa na kaunti ya Mombasa ambayo ina uwezo, kwa sababu ulimwengu mzima uendeshaji wa feri unafanywa na watu wa kaunti au serikali ndogo ndogo za pale wanakoishi. Hivi sasa, inataka kufanywa kuwa shirika halafu iwe idara katika Shirika la KPA. Tunapinga hilo kwa sababu haitafaa wala haitatusaidia. Ikiwa KFS itabidi itolewe, basi Serikali isiwe na mamlaka yoyote juu yake. Ninapendeza isimamiwe na Serikali ya Kaunti ya Mombasa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}