GET /api/v0.1/hansard/entries/1033648/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1033648,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033648/?format=api",
    "text_counter": 265,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Najiunga na wenzangu kumpa kongole Sen. Sakaja, Seneta wa Nairobi, kwa Ripoti ya ufasaha na utendakazi ambayo ameweza kuitoa. Ningependa kushauri kuwa, wale ambao wametoa ardhilhali wakati wamepeleka mashtaka mahakamani, wangeshauriwa kuondoa mashtaka yale mahakamani kwa muda. Kwa Kiingereza wanasema: Withdraw the proceedings, amaby o inakupa fursa ya kuleta mashtaka yale kortini baadaye wakati utaona kwamba labda juhudi za Kamati ya Seneti hazikuweza kufua dafu. Watakapoondoa mashtaka yale Kortini, wataweza kupata fursa baada ya muda, iwapo Kamati haikuweza kutoa mwafaka mzuri wakaweza kufuatilia maswala yale kule kule mahakamani, ambapo alikuwa ameenda awali."
}