GET /api/v0.1/hansard/entries/1033704/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1033704,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033704/?format=api",
    "text_counter": 321,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Orengo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 129,
        "legal_name": "Aggrey James Orengo",
        "slug": "james-orengo"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, ukizingatia hali yetu kama taifa, Rais, kama yule ambaye amepewa jukumu la kuongoza nchi na kusimamia mambo fulani katika Serikali, ni lazima akija hapa Bungeni aelezee haya maneno. Katika kutoa hiyo Hotuba, aliangazia mambo mengi. Katiba imeeleza ya kwamba wakati wote akija kutoa Hotuba katika kikao cha pamoja cha Bunge la Taifa na Seneti, ni lazima azungumzie mambo mawili ambayo ni muhimu. Jambo la pili ni kuhusu mambo ya kitaifa. Ukiangalia eneo la Afrika Mashariki pamoja na Afrika Kusini, yale ambayo yanaendelea kwa nchi hizi ambazo kwa kiingereza wanasema “ Horn of Africa ”, tumekuwa na matatizo mengi. Eneo hili lina watu kadri 300 milioni. Kenya lazima iendelee kuwa taa ambayo inawaka kamili. Taifa kama vile Ethiopia lina matatizo makubwa sana. Kama Kenya haitakuwa na amani, tutakuwa na matatizo zaidi katika eneo hili la Afrika. Mimi naomba Kenya iendelee kuwa na demokrasia. Hii ni kwa sababu tofauti ya Kenya na nchi zingine sita au saba katika uongozi ni kwamba, tunajaribu zaidi kuliko nchi zingine kidemokrasia. Jambo la pili ni kuwa Rais alizungumzia kwa makini yale maadili yaliyo kwenye kipengele cha kumi cha Katiba. Hayo ni muhimu kwa sababu kuna mambo ambayo yametajwa hapo kama haki za kibinadamu na mambo ya uzalendo. Rais akija katika Bunge la Taifa na Seneti, anatakiwa kuzungumzia mambo hayo kwa makini, kuonyesha Serikali yake imefanya nini kuhusu hivi vipengele vya Katiba ambavyo ni muhimu. Pia Rais aliongea kuhusu COVID-19, akisema kwamba, imetuletea madhara mengi sana. Nataka kusema bila kuogopa kwamba, Serikali ya Kenya imejaribu. Tukilinganisha na mambo yanayoendelea katika nchi kama Amerika, India au Brazil, kila nchi ina matatizo. Kenya tumekuwa na matatizo ambayo tumezungumzia, lakini ninaweza kupatia Serikali ya Kenya hongera kwa kiwango ambacho tumeweza kuyatatua. Tumeshughulikia mambo ya madhara ya COVID-19. Hivyo sio kusema ya kwamba hatukuwa na matatizo. Kuna madaktari na wale wengine ambao wanafanya kazi kwa hospitali na zahanati, ambao wengine wamekufa na wengine kupata madhara mbali mbali. Tunasema, pole kwa familia ambazo zimepoteza madaktari ambao ni ndugu zetu na watoto wetu. Tunaomba kwamba wale ambao wamekufa kutokana na madhara ya COVID-19, Mwenyezi Mungu awaweke mahali pema peponi. Lakini kuna mengi ambayo tunaweza kujaribu kufanya. Kwanza, Serikali Kuu lazima ipeleke hela za kutosha katika kaunti. Kuna kaunti ambazo zimejaribu, lakini hazina hela au vifaa. Na hii ni kwa sababu Serikali kuu ‘inakalia’ hela ambazo zinatakiwa kuenda kwa kaunti. Pia magavana wengine hawafanyi kazi vilivyo. Wako na haraka sana ya kujenga mijengo tofauti au kuangalia vile watapata kandarasi na mambo kama hayo, lakini kutoa huduma kwa wananchi imekuwa duni katika kaunti zote. Hii lazima ilete muamko katika kaunti zetu kwa sababu kutegemea hela za Serikali Kuu inalingana na Katiba, lakini Serikali za kaunti lazima zijitahidi ili wawe na hela, ambapo ikiwa kuna mambo ya hadhara kama haya, wanaweza kuitumia kuwasaidia wananchi, lakini sio kama sasa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}