GET /api/v0.1/hansard/entries/1033705/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1033705,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033705/?format=api",
    "text_counter": 322,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Orengo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 129,
        "legal_name": "Aggrey James Orengo",
        "slug": "james-orengo"
    },
    "content": "Tukiangalia mambo ya uchumi, tuko katika hali duni. Niliskia Bw. Spika wa Muda akizungumzia kuhusu mambo ya madeni. Mambo ya madeni lazima tuyaangalie. Tukianza kusikia kwamba World Bank na IMF wameanza kurudi Kenya, lazima tujue kwamba, tumeingia katika hali ya hatari. Wakati Rais Kibaki alipochukua usukani, pole pole, tulianza kuona mambo ya IMF na Word Bank yakienda chini. Lakini kwa miaka miwili iliyopita, tumeanza kusikia mambo ya IMF na World Bank. Hii inaonyesha kwamba tunaendelea kukaliwa na hizi nchi ambazo zimeendelea, na wanajaribu kuleta ukoloni mamboleo. Lazima tufanye juhudi kuona kwamba Uhuru wetu si uhuru wa kisiasa pekee yake, lazima tuwe na uhuru wa kiuchumi. Naomba Serikali Kuu ijaribu kuona ya kwamba, haya mazoea ya kuenda kutafuta madeni kila mara, lazima tujifunze kujitegemea. Bila kujigetemea, hatuwezi kuwa na Uhuru kamili. Bw. Spika wa Muda, jambo langu la mwisho ni kwamba, miaka miwili na nusu iliyopita, tulichagua Serikali. Wengi wetu walisema kwamba kulikuwa na matatizo katika uchaguzi, lakini baadaye tukakubali kwamba kuna Serikali iliyochaguliwa na watu wa Kenya. Na hiyo Serikali ikawa na nguvu zaidi wakati ambapo Rais na Mhe. Raila Amolo Odinga waliposhikana mkono mwezi wa Machi 2018. Nataka kusema bila kuogopa kwamba, kuna watu ambao wako katika chama tawala na wako kwa Serikali. Wanafaa kuamua kama jambo la muhimu kwa Wakenya ni mambo ya 2022 ama kutumikia Serikali ambayo wako ndani. Hao watu, kila siku wakienda kwa magazeti au wakitoa hotuba kwa mazishi, ni kulilia yale ambayo yanaendelea na ni wao ambao wanakaa katika Baraza ya Mawaziri. Ukienda katika ofisi za Serikali, wao ndio wako ndani ya hizo ofisi. Lakini kila siku wanalia na kusema kwamba, kuna matatizo fulani au Serikali haifanyi kazi vizuri. Sasa, ni serikali gani hiyo ambayo itafanya kazi vizuri kama hao ndio wako kwa hiyo Serikali, wanaitumikia na wana vyeo vikubwa. Bw. Spika wa Muda, unaweza kukumbuka wakati Rais wa Jamhuri ya Kenya alikuwa ameenda kule Hague, ni nani aliwachiwa mamlaka kama Kamu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya? Haikuwa Raila Amolo Odinga ama James Orengo. Mimi kama ningewachiwa mamlaka siku mbili au tatu, ningekuwa na moto kweli kweli. Lakini kila siku, hao watu wanasema mambo haya na yale kuhusu Serikali. Wakati ni huu waamue kama wako katika Serikali ama wako nje ya Serikali. Waamue wawe watumishi wa Kaisari ama sio watumishi wa Kaisari. Kwa hivyo, huu ni unafiki mkubwa sana. Hakuna kosa kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko unafiki. Mnafiki ana sifa tatu; anapenda kusema uongo. Tukianza kuangalia maneno ambayo hawa watu wanasema kila siku, ni uongo mtupu. Ukipatia mnafiki chochote kama amana ya kwamba unaenda safari, ukirudi utapata kwamba haiko kama ulivyompatia. Utapata kama imeliwa, hata kama ni hela. Utapata hela imeenda."
}