GET /api/v0.1/hansard/entries/1033710/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1033710,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033710/?format=api",
    "text_counter": 327,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Orengo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 129,
        "legal_name": "Aggrey James Orengo",
        "slug": "james-orengo"
    },
    "content": "huchagauliwa kwa miaka miwili pekee. Rais huchaguliwa kwa miaka minne wala si mitano. Uchaguzi mwingine hufika pindi tu mtu ameanza kazi. Sisi huwa miaka mitano kabla ya uchaguzi mwingine. Kwa nini hao wenzetu wasiwe na subira ya kungoja wakati ufike ndio waanze misukosuko ya siasa za 2022? Kulingana na Hotuba yake, Rais anataka tufanye kazi. Kenya imekuwa mfano mzuri kwa nchi zingine. Tulionyesha kwamba tunaweza kupigana kwa sababu ya uchaguzi lakini baadaye tukafanya kazi pamoja kwa sababu Kenya ina Serikali moja. Hata upinzani ni moja tu. Katika hii Seneti, mimi ndiye Kiongozi wa Wachache. Upande ule kuna Sen. Poghisio ambaye tunafanya kazi naye vizuri. Si kazi ya kupiga tu makofi. Huwa tunajieleza kama kuna mambo ambayo hatukubaliani nayo. Kule Marekani kuna mtu anayeitwa Pence. Huwezi kusikia akisema kitu tofauti na Trump ambaye ndiye Rais. Najua kuna tabia zingine za Trump ambazo hapendi hata kidogo yeye kama Mkristo. Kwa sababu alichagua kufanya kazi na Trump kama makamu wake, lazima afuate kanuni ambazo walikubaliana wakati wa uchaguzi. Bw. Spika wa Muda, sitaki kusema mengi sana. Kwa miaka miwili ambayo imesalia, tunafaa kutunga sheria inayohusiana na maelewano kati ya Raila Amollo Odinga na Rais Uhuru Kenyatta. Wale wanaotaka viti wangoje mpaka uchaguzi ufanyike ili tuone nani atakuwa mshindi. Kwa sasa, kazi yetu kubwa ni kuleta amani katika nchi yetu ya Kenya. Kuanzia kesho tutakusanya mamilioni ya sahihi za Wakenya na nina imani tutapata. Nina uhakika tutapata sahihi zaidi ya milioni nne kwa sababu tuko wengi sana. Najua tutapata sahihi kutoka kaunti zaidi ya 40. Kwa wale waliokuwa wakifiria reggae ilisimama, mwezi wa nne mwaka ujao tutakuwa na Referendum. Najua Seneta wa Nairobi anafahamu mchezo wa reggae na pia aneweza kucheza gitaa. Hata hivyo, najua tutafika na tutafaulu. Asante Bw. Spika wa Muda."
}