GET /api/v0.1/hansard/entries/1033763/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1033763,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033763/?format=api",
    "text_counter": 380,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "vile, ningependa kumpa kongole kwa zile ripoti nne ambazo aliweza kutoa katika Bunge kama inavyosema Katiba yetu. Hii ni mara ya tatu katika Bunge hili kwa Mhe. Rais kuja kuhutubia Bunge. Kila anapokuja kuhutubia Bunge huwa anatoa ratiba ya zile kazi ambazo Serikali yake imeweza kufanya kwa muda huo mpaka pale hali ilipofika kufikia sasa. Bi Spika wa Muda, nitagusia mambo matano ambayo Rais ameweza kuzungumzia katika Hotuba yake. Kwanza kabisa nitaanza na swala la usalama. Rais alieleza kuwa swala la usalama wa nchi ni mzuri sana na hakuna jambo lolote ambalo linaweza kuchukuliwa kama la kutishia kama usalama wa nchi. Tukiangalia hapo nyuma tulikuwa tumezungumzia visa vya watu wasiojulikana kuvamia na kuua watu kiholela. Kwa mfano kule Kwale kumetokea visa kadhaa ambapo watu wameweza kuuliwa na wengine wakatekwa nyara na maiti zao kupatikana baadaye bila ya kupata maelezo yoyote kuhusiana na visa hivi. Bi Spika wa Muda, katika Bunge hili, niliweza kuleta ripoti kwamba watu wasiojulikana walivamia makaazi katika Chuo cha Kiislamu kule eneo ya Kilifi na kuteka nyara watu wane. Watatu waliachiliwa lakini moja mpaka leo hajulikani alipo. Inasikitisha kwamba wakati tunaelezwa kuwa hali ya usalama ni nzuri katika nchi yetu ya Kenya, bado kuna visa vya watu kupotea kiholela na wengine kuuliwa bila kutoa maelezo yoyote kuhusiana na maswala haya. Bi Spika wa Muda, ningependa labda katika maelezo yajayo Mhe. Rais aweze kugusia swala hili la watu kupotezwa ama kuuliwa kiholela katika nchi yetu ya Kenya, wakati sisi tuna Katiba ambayo inalinda haki za binadamu na tumeweka sahihi mikataba mingi ya kimataifa kuhusiana na haki za binadamu. Jambo la pili ni swala la afya. Rais aligusia kuwa Universal Health Coverage (UHC) karibuni itakuwa inatumika katika nchi nzima katika Jamhuri yetu ya Kenya. Tuliona pia kwamba amegusia swala la ugonjwa wa COVID-19 ambao umeathiri ulimwengu mzima kwa jumla. Bi Spika wa Muda, lakini jambo la kusikitisha ni kuwa hapa katika nchi yetu ya Kenya hatujaweza kutilia mkazo zaidi kuhusiana na matibabu au vipi tutapambana na ugonjwa huu wa COVID-19. Tukiangalia wale madaktari wenye uzoefu mkubwa, umri wa wengi wao ni zaidi ya miaka 55, ambapo hawaruhusiwi kwenda kazini mara kwa mara. Tunabaki na madaktari ambao hawana tajriba ya kuweza kupambana na ugonjwa huu. Unapata kwamba wengi wao ni vijana na bado wana uoga wa kuweza kufanya kazi kikamilifu. Bi Spika wa Muda, ningependa kusema kwamba mbali na kupewa vifaa vya kujikinga na ugonjwa huu, madaktari wanatakikana kupewa ushauri nasaha mara kwa mara kwa sababu maradhi haya yanaathiri sio wao pekee, bali hata familia zao kwa sababu wanapotoka kwenda kazini, haijulikani kama watarudi na ugonjwa ama watakuwa wazima. Lazima swala hili la ushauri nasaha kwa madaktari ufanywe. Vile vile, wanafaa wapewe marupurupu yao kwa wakati unaofaa. Hali zao za kufanya kazi zinafaa ziimarishwe ili kuhakikisha kwamba madaktari, wauguzi na wengine wanaohusika na kutibu na kuangalia wagonjwa wa COVID-19 wanaweza kuangaliwa kwa njia mzuri. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}