GET /api/v0.1/hansard/entries/1033764/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1033764,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033764/?format=api",
"text_counter": 381,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bi Spika wa Muda, jambo la tatu ni swala la vita dhidi ya ufisadi. Ufisadi umerejea tena upya katika nchi yetu. Tukiangalia matumizi za pesa za COVID-19 na utoaji wa zabuni katika Kenya Medical Supplies Authority (KEMSA), yote haya ni maswala ambayo yako wazi, ambapo Rais angeweza kuyazungumzia kwa ufasaha zaidi. Bi Spika wa Muda, hapo nyuma, Rais alikuwa ametoa ilani ya siku 21 kwa Directorate of Criminal Investigations (DCI) na Ethics and Anti-Corruption Commission (EACC) kuhakikisha kwamba wale ambao wamekula pesa za KEMSA ambazo zilinuiwa kusaidia katika vita dhidi ya COVID-19 katika nchi yetu ya Kenya washtakikwe na wapelekwe mahakamani haraka iwezekanavyo. Hadi leo, hakuna jambo lolote ambalo limefanywa. Faili inapelekwa kwa Director of Public Prosecutions (DPP) kisha inarejea kwa DCI. Hii inapoteza wakati na wale ambao wameweza kupata pesa hizo wanaendelea kuzitumia. Zile pesa zitatumika kulipa wale ambao watakuja kuwatetea katika muhula ujao wa kura. Bi Spika wa Muda, swala la ufisadi limekithiri sio katika Serikali kuu pekee yake, lakini hata serikali za county. Tuliona zile pesa ambazo zilipelekwa kupambana na COVID-19 katika kaunti; zote hazikuweza kutumika kisawasawa. Mpaka leo, hakuna kaunti yoyote ambayo inaweza kusema kwamba wao wameweza kujimakinisha na wanaweza kupambana na vita dhidi ya COVID-19 kwa uwezo ambao tulipewa na Serikali. Nimeweza kuzuru Kaunti za Isiolo, Meru, Mombasa, Kilifi na Kwale. Kote, tuliona kwamba kuna upungufu mkubwa wa vifaa vya kupambana dhidi ya ugonjwa wa COVID-19. Hii ni kwa sababu pesa zimeletwa lakini hazikutumika kisawasawa kulingana na vile ambavyo inatakikana. Bi Spika wa Muda, Hotuba ya Rais pia ilizungumzia maswala ya ujirani mwema. Rais aliomba kwamba majirani wetu wafuate mfano wetu kuweza kushikamana kupitia kwa “ Handshake ” na kuleta uwiano katika vyama vya kisiasa. Hiyo ni ili tuone kwamba watu wanaendelea kuishi kwa amani na upendo. Mambo yaliototokea katika Jamhuri jirani ya Tanzania wakati wa uchaguzi mkuu wao uliofanyika mwezi uliokwisha ni ya kusikitisha. Kulikuwa na visa vya watu kuuliwa kule Pemba, Zanzibar na hata Dar-es-Salaam. Watu waliweza kupigwa na kuumizwa vibaya wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge katika Jamhuri ya Tanzania. Bi Spika wa Muda, sote tuko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Sote tumeweka mikataba ya kuhakikisha kwamba nchi zetu zinaongozwa kwa sheria na utangamano. Lakini yale yaliyoibuka Tanzania na Uganda hivi juzi yanaleta shaka katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ni vipi tutaweza kukosoana wakati wenzetu wameweza kuteleza na kufanya mambo ambayo ni kinyume na demokrasia. Hayo yote nikiyazungumzia ni kwamba sisi sote katika Afrika Mashariki, tuna nia ya kuwa na ile tunaita kwa Kiingereza “federation”. Yaani, nchi zote za Afrika Mashariki zinaongozwa na mfumo mmoja wa serikali ama kiuchumi. Bi Spika wa Muda, itakuwa sio sawa wakati sisi tunasonga mbele kuhakikisha kwamba uhai wa binadamu unalindwa na wenzetu katika Tanzania na Uganda bado wako The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}