GET /api/v0.1/hansard/entries/1033765/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1033765,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033765/?format=api",
"text_counter": 382,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "katika enzi za chama kimoja na wapinzani kupigwa na wengine kuumizwa kwa sababu ya maoni yao ya kisiasa. Hili swala la uhusiano na nchi za nje, lazima Serikali yetu iliingalie. Wale wanapigwa Tanzania ni kwa sababu ya maoni yao ya kisiasa. Hawapigwi kwa sababu wameweza kuvunja sheria. Bi Spika wa Muda, nikiongezea, kuna kisa ambacho mtu aliuliwa hivi juzi kwa sababu alipigwa na wanajeshi kule Tanzania na ana familia yake katika eneo la Mombasa. Ilikuwa ni jambo la kusikitisha kwamba mtu amepoteza maisha katika mikono ya Serikali na hakuna jambo lolote ambalo ataweza kufanya kulingana na sheria zao. Swala la demokrasia katika eneo letu la Afrika Mashariki ni lazima tulitilie mkazo. Hii ni kwa sababu kukitokea misukosuko ya kisiasa kama hii inayotokea katika upande wa Ethiopia, inabidi watu wahame makao na waende katika nchi jirani kutafuta makao mapya. Sisi kama Kenya, tumekuwa ni nchi ambayo imekuwa na amani na inawapa watu wengi fursa kuweza kujificha hapa wakati nchi zao zina misukosuko za kisiasa. Bi Spika wa Muda, kumalizia ni kuwa Rais pia alizungumzia maswala ya uchumi. Ijapokuwa uchumi wetu ulikuwa umeonyesha ishara za kuanza kufufuka, uliweza kupigwa vibaya na janga la COVID-19. Ninampongeza kwa miradi ambayo ameweza kuitoa ili kuweza kusisimua uchumi wetu ili uweze kusimama. Jambo ambalo linasikitisha ni kuwa, kwanza ufisadi bado uko katika Serikali. Kwa hivyo, zile miradi zote ambazo zinanuiwa kufanyika ili kufufua uchumi wetu zinazingirwa na ufisadi. Hii ni hali ambayo inatoa fursa duni kwa wale wahusika kuweza kusonga mbele. Bi Spika wa Muda, vile vile, hii ina maana kwamba, ni vigumu pia kwa biashara kuweza kufufuka kwa sababu ya uwezo wa wananchi kununua bidhaa, kwa mfano, uwezo wa wananchi kuenda katika mahoteli, kuzuru mbuga za wanyama na kuzuru ufuo wa bahari ili kujivinjari umepungua. Hii ni kwa sababu mapato yamepungua. Ningependa kusema kuwa, Serikali iweze kurudi tena na kupanga mikakati zaidi ili kuweza kuinua uchumi wetu ili wananchi waweze kupata ajira na vile vile pesa mikononi mwao, ili waweze kutumia na kufufua uchumi wetu uwe mzuri zaidi. Bi Spika wa Muda, shule zinafunguliwa Januari. Lakini hatujajitayarisha kwa vyovyote kuhusiana na maswala ya kufungua shule. Kama ilivyo sasa, tuliambiwa kwamba hospitali zimetayarishwa na kila kaunti iko tayari kupokea wagonjwa wa COVID-19. Lakini ilipokuja awamu ya pili ya COVID-19, wengi wameanza kutapatapa. Inasikitisha kwamba, utapata hospitali nyingi hazina hata kitanda kimoja cha kuhudumia mgonjwa wa COVID-19. Bi Spika wa Muda, katika nchi yetu ya Kenya, kuna mengi ambayo yunaweza kufanywa. Kama alivyozungumzia Sen. (Dr.) Zani kuwa Serikali kuu inaingilia huduma ambazo zinatolewa na kaunti, kwa mfano, huko Mombasa, feri sasa inarejeshwa katika Kenya Ports Authority (KPA). Baada ya kutolewa kwa Kenya Ferry Services (KFS) iingie katika mkono wa Kaunti ya Mombasa, sasa inakuwa ni kitengo katika KPA ambacho kazi yake hususan ni kushikisha na kupandisha mizigo katika meli katika Jamhuri yetu ya Kenya. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}