GET /api/v0.1/hansard/entries/1033772/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1033772,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1033772/?format=api",
    "text_counter": 389,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Omogeni",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13219,
        "legal_name": "Erick Okong'o Mogeni",
        "slug": "erick-okongo-mogeni"
    },
    "content": "Bi Spika wa Muda, nafikiri kwa sababu leo ilikuwa siku ya sisi Maseneta kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili, mimi pia nitatoa mchango wangu kwa Hotuba ya Rais kwa lugha ya Kiswahili. Kwanza kabisa natoa shukrani zangu kwa Rais wa Taifa kwa ile Hotuba ambayo alitoa kwa Bunge zetu mbili, haswa kwa yale ambayo aliweza kuzungumzia ambayo inagusia wale ambao sisi ni wawakilishi wao. Bi Spika wa Muda, nilipendela sana Hotuba ambayo Rais alitoa ambayo ilikuwa inalenga wale ambao wanataka kufanya biashara katika nchi yetu ya Kenya. Ukiangalia katika ile Hotuba ya Rais wetu wa Taifa, aliweza kueleza kwamba, katika nchi nyingi sasa, Kenya ni kati ya mataifa ambayo yameweka sheria ambayo imefanya kusajili makampuni kuwa kazi rahisi sana."
}