GET /api/v0.1/hansard/entries/1034432/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1034432,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1034432/?format=api",
"text_counter": 217,
"type": "speech",
"speaker_name": "Baringo CWR, KANU",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Gladwell Cheruiyot",
"speaker": {
"id": 13231,
"legal_name": "Gladwell Jesire Cheruiyot",
"slug": "gladwell-jesire-cheruiyot"
},
"content": " Ahsante sana kwa nafasi hii umenipa niweze kuchangia Hoja hii inayoendelea wakati wa sasa, kuhusiana na wale watu ambao wako na changamoto ya miili yao, jinsi ambavyo wako na ulemavu. Jambo hili linaguza kila mtu. Ni jambo ambalo kila mtu anahitaji kulitilia maanani. Katika nchi hii, tunapopanga kazi na ratiba zetu kila wakati, ni vyema tuwe tukiwakumbuka wale wenzetu wanaoishi na ulemavu. Hata tunapoongea mambo ya ulemavu, ni kweli kwamba huduma za afya nchini humu zimegatuliwa. Kule mashinani katika kaunti zetu wangeweza kuweka bajeti ya kuhudumia watu hao. Wakati tunaposema BBI itaweka fedha nyingi kwa kaunti zetu, ningependa kaunti zitilie jambo hili maanani, maanake kule ndiko wanaweza kujua idadi ya watu walioko katika wadi zao na wale walemavu. Itafaa wapitishe bajeti wakiwa na idadi hiyo ndio watu wapate huduma kwa njia ambayo inafaa binadamu. Wakati mwingine tunachukulia hao watu kama kwamba hawafai. Hata unakuta kwamba wanafichwa nyumbani mwetu. Kama vile kila mtu amesema hapa, huu ni mtihani ambao kila mtu anaweza pita. Lakini wakati mwingine, jinsi ambavyo tunawachukulia walemavu si kama binadamu ama njia ambayo inamfurahisha Mwenyezi Mungu. Tukiongea hapa kuhusu vifaa ambavyo wanatumia, kuna jambo moja huko kwetu Baringo ambalo limenisumbua na nataka kulitatua. Nashangaa kama Kenya nzima iko na hiyo shida. Katika kaunti zetu, tukiangalia sehemu za biashara, ni ngapi zinavyoo vinavyo ambavyo vinawafaa walemavu? Hii ni kuonyesha hatuwakumbuki. Walemavu pia wanafanya biashara lakini hawana vyoo vinavyo wafaa. Wamama ndio wameathirika zaidi kutokana na hii shida. Kwa sababu mama akiwa na mtoto ambaye hawezi kutembea, hiyo ni shida yake. Huyu mama hubaki nyumbani na haendi shambani. Wakati mwengine unapata mama yule bado ana umri mdogo lakini amezeeka kwa sababu ya mawazo. Hana fedha za kulisha mtoto ama kununua bidhaa za kumsaidia. Sisi kama viongozi wa nchi hii tuwape kibao mbele walemavu ili waweze kuiishi kama watu wengine. Mheshimiwa ambaye ameongea mbele yangu amesema kwamba kwa muda mfupi alikuwa na ulemavu lakini sasa ako sawa. Bado anakumbuku kwa ugumu na ndio anahitaji sisi kuwasaidia walemavu. Nashukuru kwa kupata nafasi kuchangia Hoja hii kwa sababu ni nzuri. Pia nimeona wenzangu wanachangia kwa njia inayofaa. Naunga mkono mia kwa mia. Serikali ya Ugatuzi pamoja na Serikali kuu wanapaswa kuketi pamoja na kuangalia vile walemavu wataishi vyema hapa nchini. Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}