GET /api/v0.1/hansard/entries/1034443/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1034443,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1034443/?format=api",
    "text_counter": 228,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Beatrice Adagala",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13280,
        "legal_name": "Beatrice Kahai Adagala",
        "slug": "beatrice-kahai-adagala-2"
    },
    "content": "(Vihiga (CWR), ANC): Asante sana, Mhe. Naibu Spika Muda kwa kunipa nafasi hii niweze kusema jambo kuhusu huu mjadala wa walemavu. Nimesikia vile Mhe. Ghati pamoja na Mhe. Sankok wameongea. Kusema kweli, walemavu wako na shida mingi. Wengi wao hawana vifaa vya kuwasadia kutembea kama mikogonjo, viti vya migurudumu na kadhalika. Ni huzuni kubwa kwa sababu watu wengi huwaficha walemavu. Nimesikia huzuni mingi sana moyoni mwangu kusikia kuna mahali mlemavu alikuwa amefungwa kama mbuzi katika zizi la ng’ombe. Hili si jambo la haki. Mlemavu ni kama binadamu wengine. Wanafaa kulindwa kisheria na kupewa haki zao. Jambo la walemavu si la kuchukuliwa kwa mzaha, mbali lina takikana kuchukuliwa kwa makini. Mahitaji yao yanapaswa kuchukuliwa kama ya Wakenya wengine. Kusema ukweli kuna wengine ambao tangu wazaliwe hawajawahi kutembea wengine wakiwa na umri wa miaka 50 ama 60. Wengine wanafaa kupewa nepi. Kusema ukweli, huko vijijini vya kwangu kuna wamama ambao hawawezi kununua hizo nepi. Walemavu wanafungwa matambara na vidonda za kitanda zinawashika na wako tu. Kwa hivyo, wanahitaji usaidizi unaofaa. Serikali inapaswa kuhudumia ndugu zetu na baba wetu ambao ni walemavu. Nimeona dada yangu, Mhe. Ghati, ameongea kwa upendo. Tumetembea naye katika mikutano mingi. Naona mama anatetea walemavu na ukiangalia, hakuna mtu ambaye angependa kuwa na mlemavu. Yeye ni kiumbe au mtu ambaye Mungu aliumba kama wengine. Wanafaa wapewe mahitaji yao vile wanavyohitaji. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}