GET /api/v0.1/hansard/entries/1034444/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1034444,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1034444/?format=api",
"text_counter": 229,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Beatrice Adagala",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13280,
"legal_name": "Beatrice Kahai Adagala",
"slug": "beatrice-kahai-adagala-2"
},
"content": "Kuna zeruzeru ambao wanahitaji mafuta ya kujipaka ndiyo jua lisichome sana ngozi yao na tena wanahitaji miwani kwa wingi. Nasihi serikali iangalie tuone mahitaji ya hawa ndugu, dada na baba zetu wanalindwa katika hii nchi yetu ya Kenya. Na ifanyike haraka tuone kwamba inashughulikiwa vilivyo na walemavu wote katika nchi hii wanashughulikiwa. Nikiongea hivi, tumejaribu kununua wheelchairs na hazitoshi. Unajaribu kutoka kwa mfuko wako lakini hazitoshi. Ukienda kwa hafla tofauti unaona mzee au mama anakuja akitambaa chini. Hawa watu wanahitaji waishi maisha ambayo yanafaa katika hii nchi yetu ya Kenya. Kwa hivyo ningependa kuunga mkono Hoja hii na kusema kwamba walemavu wapewe nafasi kimasomo, kibiashara na kimaisha. Waishi kama wakenya in a dignified manner. Asante sana, Mhe Naibu Spika wa Muda."
}