GET /api/v0.1/hansard/entries/1034471/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1034471,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1034471/?format=api",
    "text_counter": 256,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taveta, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": " Yes, I am getting there. Bi. Naibu Spika wa Muda, nimeanza kwa kutaja kuwa aliyeleta Hoja hii amefanya jambo muhimu sana. Ningetaka kuunga mkono Mhe. Daktari James Nyikal ambaye tuliweza kufanya kazi pamoja na walemavu hapa nchini. Sioni aibu kusema kuwa alikuwa Katibu wangu wa Kudumu na alipigania swala la walemavu vilivyo. Ukweli ni kwamba walemavu wanateseka hapa nchini. Na katika hali ya mateso yale, kuna umuhimu wa sisi kujua kuwa Kipengele cha 27 cha Katiba ya Kenya kinasema tusibaguane. Tusibague mtu kwa misingi ya ulemavu, dini, kabila au rangi. Haya yote yametajwa katika Katiba yetu. Hivyo basi, ninakubaliana na kuunga mkono kuwa kuna umuhimu wa sisi kufanya uamuzi ambao utaweza kutekelezwa na Serikali kuu ya hapa nchini. Ni kweli kwamba uamuzi wa swala lolote ambalo linagusia pesa ambazo zinatakiwa kutumika kutoka kwa Serikali Kuu - kuna umuhimu wa kukumbuka kuwa Katiba hii pia inatueleza kuhusu suala hili - ni lazima lipitie mikakati fulani. Tujue kuwa walemavu ni wenzetu hapa nchini na wana haki ya kupata usaidizi kama ule wa viti vya magurudumu, mikongojo, bakora wanazozitumia na vifaa vingine vya kuwasaidia. Wao pia ni watoto wetu na ni wenzetu. Wanalipa ushuru kama wanavyolipa wengine hapa nchini. Basi, tuna haki ya kufanya uamuzi kuwa Serikali Kuu ni lazima iwalinde na kuwapatia vifaa hivyo vya kuwawezesha. Bi. Naibu Spika wa Muda, namuunga mkono Daktari James Nyikal kwa kuleta pendekezo hilo ijapokuwa mikakati ile inapaswa kufuatwa. Tunapopitisha swala hili, tulipitishe moja kwa moja ili tuweze kuhakikisha kuwa ndugu zetu wanaoishi na ulemavu wanaweza kupata usaidizi. Kwa hayo machache, naunga mkono."
}