GET /api/v0.1/hansard/entries/1034631/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1034631,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1034631/?format=api",
"text_counter": 109,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisumu Magharibi, FORD-K",
"speaker_title": "Hon. Olago Aluoch",
"speaker": null,
"content": " Mhe Spika, ningependa kumuuliza Waziri wa Uchukuzi, Miundo-msingi, Makaazi, Usitawi wa Miji na Ujenzi wa Miradi ya Umma: (i) Je, Waziri anaweza kufafanua sababu za Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ya Kenya kufunga Barabara ya Usoma-Nawa-Kirembe (C-35) kwa kujenga ukuta ili kulinda sehemu ya kusini ya eneo la ndege la Kisumu, bila kutoa barabara mbadala hivyo kuwatatiza wakaazi kufika makwao kwa kupitia mojawapo ya sehemu mbili za uwanja wa ndege? (ii) Je, Waziri ana habari kuwa karibu shilingi milioni 45 zilitengwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ya Kenya ili kuwezesha ubunifu na ujenzi wa barabara mbadala sambamba na barabara ya C35 iliyofungwa, ilhali mamlaka hiyo inadai kwamba pesa hizo hazikutumika kwa kazi hiyo ambayo zilitengewa? (iii) Ni hatua zipi Waziri amechukua ili kuratibu mipango ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndenge ya Kenya na Mamlaka ya Barabara za Mijini ya Kenya ya kubuni na kujenga barabara ya C35 ili watu wapate nafasi ya kupitia wanapoenda kwenye makazi yao? Hiyo barabara lazima iinuliwe ili isiharibiwe na kuongezeka kwa viwango vya maji ya Lake Victoria."
}