GET /api/v0.1/hansard/entries/1034898/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1034898,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1034898/?format=api",
"text_counter": 376,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Asante sana, Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii nami pia nizungumzie swala hili nyeti. Hii ni Hoja inayoleta taarifa kuhusu makadirio ya pesa iliyopeanwa kutoka wizara tofauti tofauti. Vile vile, Kamati ya Bunge itueleze kuhusika kwenye makadirio ya kuhakikisha kuwa zile pesa tulizokuwa tumekadiria tuliweza kuzibadilisha zitumike kwenye janga hili. Sio siri kwamba kuna utukutu mwingi katika nchi hii. Wafanyibiashara wasiokuwa na nia nzuri walitumia janga hili kujinufaisha. Kamati ya Bunge inayosimamia masuala ya afya imezungumza kinaganaga juu ya matatizo yaliyoko, haswa, zile pesa zilizofujwa badala ya kutumika vile ilivyotakikana. Ni dhahiri kwamba wale waliofanya biashara na KEMSA hawakujua Wakenya wanahitaji usaidizi kwenye janga hili. Wahudumu wa afya wanajikaza ili Wakenya wapate huduma. Eneo langu la uwakilishi Bungeni liko mpakani. Tuko na shida ya Coronavirus kutoka nchi jirani na pia kwetu kwenyewe. Tumepigika sana. Ni shida kubwa iliyoko kule kwa sababu mtu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}