GET /api/v0.1/hansard/entries/1034899/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1034899,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1034899/?format=api",
"text_counter": 377,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "akija hospitali akose kivuta pumzi, hata kama haugui Coronavirus, hawezi kusaidika maanake hawawezi kupata njia ya kupata hewa ya haraka ili atibiwe. Wakenya wako na shida kubwa sana. Ninashangaa kuwa mtu anaweza kulala usingizi akijua amechukua pesa amezifuja kwa ufisadi na kuweka mfukoni na kulala akifikiri ametajirika ama akitarajia kuwa wanawe wanatakikana kuishi vizuri kuliko Wakenya wengine. Ni jambo la aibu na la kusikitisha. Ninatumai kufikia sasa watu waliohusika wangekuwa wakichezea jela, kama kweli kuna vita dhidi ya ufisadi humu nchini. Ni laana na dhambi. Nilimuona aliyekuwa Katibu wa Kudumu tuliyefanya kazi naye, Dr. Nyikal, na ambaye pia ni daktari, akibubujikwa na machozi. Watu wengine walifikiri ni utani. Jambo hili si la utani. Ni la ukweli. Alizungumza kwa uchungu. Na hayo ndio machungu yanayokumba Wakenya wengi, haswa, tukiwa viongozi tukijua kuwa mikono yetu imefungika. Tunashindwa vile tutawasaidia wananchi, haswa kwa sababu Mhe. Nyikal mwenyewe ni daktari. Yeye alizidiwa zaidi kwa sababu ya ule uzito na shida aliyoiona na kutokuwepo na uwezo wa hao watu kusaidika. Vifaa ambavyo wafanyikazi wa Afya wangetumia kujikinga havijatumika. Wauguzi wanakufa kama nzige. Hili ni jambo la kusikitisha sana. Ninaunga mkono taarifa hii lakini juu ya hapo, wacha nimalizie kwa kusema kuwa ni lazima watu waadhibiwe. Asante."
}