GET /api/v0.1/hansard/entries/1036945/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1036945,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1036945/?format=api",
    "text_counter": 313,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "wako na umri kati ya miaka 30 na 45. Kwa hivyo, hawana tajriba ya kutosha kuweza kutibu na kuangalia wagonjwa kama hao. Nikizungumzia Mombasa, nimewahi kuzuru hospitali kuu ya Coast General Hospital mara tatu kwa muda wa wiki mbili ili kusaidiana na watu waliofiwa, kuweza kuchukua miili zao. Ni jambo la kusikitisha kwamba unapopelekwa katika wadi ya COVID-19, huo unakuwa mwisho wa mawasiliano yako na jamii yako na huenda ukapoteza maisha bila ya kuwa karibu na jamii yako kuweza kukuombea dua ama kukuombea Mungu ili safari yako, unapokwenda, iwe ya salama. Bi. Naibu Spika, tunaona kwamba madaktari, bali na kuwa wanafanya kazi katika hali ngumu, hawalipwi mshahara wao na marupurupu yao kwa wakati unaofaa na hii inawatoa morale ya kuweza kufanya kazi hususan wakati huu ambapo tuna janga la COVID-19. Wale madaktari ambao wanatibu wagonjwa wa COVID-19 wanahitaji ushauri nasaha ili waelezwe kwamba haya matatizo yako na binadamu---"
}