GET /api/v0.1/hansard/entries/1036948/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1036948,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1036948/?format=api",
"text_counter": 316,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante Bi. Naibu Spika. Kitu cha kwanza, ni jambo la kusikitisha yale ambayo yalifanyika huko Kapkatet ambapo mtu ambaye hakuwa amefariki alipelekwa pahali pa kuekwa maiti. Huu mgomo ambao unakuja Jumatatu wa madaktari ni kwa sababu madaktari wanafanya kazi katika hali ngumu, ilhali mishahara yao ni ndogo. Kuepukana na mgomo kama huu ni muhimu kwa sababu huu wakati wa COVID-19 ni wakati mgumu kwa wananchi. Ikiwa madaktari hawataweza kupatikana ama watajitenga kando, wale watu ambao watakua wanalindwa katika zile mashine watakua wapi? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}