GET /api/v0.1/hansard/entries/1037023/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1037023,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037023/?format=api",
"text_counter": 391,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Mhe. Spika wa Muda, kwanza naipongeza Kamati kwa hiyo Ripoti yake, lakini masikitiko ni kwamba Kamati hii haijaangazia Taarifa yangu ambayo nilileta hapa Tarehe 24 Mwezi wa Tano mwaka huu kuhusiana na kuangushwa kwa ndege ya Kenya nchini Somalia. Ndege ile ilikuwa ya Shirika la African Express Airways ambayo ilipigwa ikiwa inatua katika uwanja mmoja nchini Somalia. Mwezi uliopita pia nilipewa fursa kuikumbusha Kamati hii kwamba hiyo Taarifa bado haijajibiwa na kwamba tunahitaji majibu kwa haraka kwa sababu kuna ripoti inayotakikana kutayarishwa na nchi ya Somalia ambamo ndege ilianguka. Ripoti ile itasaidia kulipwa ridhaa kwa wale waliohusika katika ajali ile ambayo marubani wawili na wasaidizi wao walipoteza maisha yao. Ni muhimu kwamba Kamati hii ilipe Bunge hili ripoti kwa ufasaha, ni lini watazingatia mambo hayo ikizingatiwa kwamba madai ya malipo kwa familia za wale waliopoteza maisha yao baada ya mwaka mmoja kutoka tarehe ya ajali. Ajali ilitokea mwanzoni mwa Mwezi wa Tano. Kwa hivyo, imebaki takriban miezi mitano kitambo madai yao yafe. Vile vile, hatujapata ripoti ambayo itatupa mwongozo ni nani wa kulaumiwa kuhusiana na ajali ile. Ningependa nipate ufafanuzi wa swala hilo."
}