GET /api/v0.1/hansard/entries/1037044/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1037044,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037044/?format=api",
    "text_counter": 412,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Sakaja",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13131,
        "legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
        "slug": "johnson-arthur-sakaja"
    },
    "content": "Nimekusomea Kipengele cha 93 katika Kanuni zetu za Kudumu na nimeona ya kwamba kumeanza kuwa na uzoefu. Nilimskia Sen. (Dr.) Zani akijaribu kuzua Hoja ya nidhamu lakini hakuskizwa. Hapo awali hata mimi nilipitia hayo. Sijui kama Kanuni hii imebadilika kwa sababu inasema kwamba Mbunge yeyote anaweza kuibua Hoja ya nidhamu wakati wowote ambapo Seneta mwingine anachangia kwa kueleza kwamba anasimama kwa Hoja ya nidhamu na atahitajika kuitaja Kanuni inayokiukwa. Hakuna mahali inasema kwamba Spika ataamua kama atampa nafasi ama hatampa kwa sababu ni haki ya huyo Seneta kuibua Hoja ambayo yuko nayo."
}