GET /api/v0.1/hansard/entries/1037045/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1037045,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037045/?format=api",
"text_counter": 413,
"type": "speech",
"speaker_name": "The Temporary Speaker",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "(Sen. (Dr.) Mwaura): Nafikiri hakuna tashwishi Sen. Sakaja kwa sababu kila mtu ambaye ameomba kutoa Hoja ya nidhamu ameweza kupatiwa nafasi ya kufanya hiyo Hoja ya nidhamu. Lakini tusiwe na ule uzoefu wa kwamba ni lazima. Seneta wa Mombasa alikuwa amesimama kwa Hoja ya nidhamu. Kwa hivyo, hauwezi ukachukua ile nafasi kumpa Seneta mwingine pia Hoja ya nidhamu kabla ile nyingine kumalizika. Kuna utaratibu wa Bunge la Seneti na hilo ndilo jukumu la Spika. Lazima Spika aonyeshe taratibu katika Bunge la Seneti. Lakini najua kuna ule uzoefu wa kwamba kuna Maseneta wengine ambao wanataka wakishaitisha Hoja ya nidhamu, wengine wanyamaze lazima kwanza yeye azungumze. Nafikiri hiyo sio haki. Kuna utaratibu ambao unafaa kufuatwa na mimi kama Spika msaidizi nina jukumu la kuhakikisha kwamba kuna nidhamu katika Bunge la Seneti. Sen. Kang’ata, endelea. Samahani kwa hilo. Nimeelekezwa ipasavyo. Nataka sasa kuweka swala rasmi kwamba:- Kutokana na Kanuni za Kudumu, Kanuni ya 31(3)(a) kwamba Bunge la Seneti liweze kuazimia kuongeza muda wa Kikao hiki mpaka mwisho wa Hoja zote, Hoja ya 19 ikiwa ya mwisho katika orodha ya Ratiba ya leo."
}