GET /api/v0.1/hansard/entries/1037065/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1037065,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037065/?format=api",
    "text_counter": 433,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Omogeni",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13219,
        "legal_name": "Erick Okong'o Mogeni",
        "slug": "erick-okongo-mogeni"
    },
    "content": "Asante sana Bw. Spika wa Muda. Nitajitahidi sana kuendelea na kumaliza katika lugha ile ya kitaifa ya Kiswahili. Nataka kumshukuru Rais kwa ile Hotuba ambayo alitoa. Hii ni kwa sababu alitueleza kwamba katika huu mwaka ambao alikuwa anatupa ripoti hii ambayo ilisomwa tarehe 12 Mwezi wa 11 mwaka wa 2020, Serikali ilikuwa imeweka mikakati ya kununua madawati ya shule 250,000. Hii ni ili kuhakikisha kwamba watoto wetu watakapokuwa wanarudi shule mwaka ujao, watakuwa na nafasi ya kuwa na ule umbali wa mita moja na nusu. Hiyo ni ili kusiwe na madhara katika shule kupitia ugonjwa huu wa Coronavirus (COVID-19)."
}