GET /api/v0.1/hansard/entries/1037067/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1037067,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1037067/?format=api",
"text_counter": 435,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Omogeni",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13219,
"legal_name": "Erick Okong'o Mogeni",
"slug": "erick-okongo-mogeni"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, hoja nyingine ambayo ningetaka kuguzia katika ile Hotuba ya Rais ni kuhusiana na jitihada ambayo Serikali yake imeweza kufanya kupigana na hili janga la COVID-19. Nakubali kwamba Rais alipoanza kushughulikia ugonjwa wa COVID-19 alianza kusaidia wakenya ambao walikuwa wanaathiriwa na hili janga. Aliweka mikakati rasmi ya kuwalinda Wakenya, haswa mambo ya kupunguza kodi na kuhakikisha kwamba watu walikuwa wanawekewa amri ya kutokutana ama kutembea kutoka kaunti moja hadi nyingine."
}